Jisome Kwanza Wewe Mwenyewe


Categories :

Moja ya kikwazo kikubwa kilichokuzua kutokupiga hatua ili kusogelea kile unachokitaka ni tabia yako ya kuwasoma watu wengine.

Umetumia muda mwingi kufuatilia mienendo ya watu wengine huku ukiacha maisha yako yajiendeshe yenyewe.

Je huwa hushituki unafahamu taarifa za mtu mwingine kiundani kuliko za kwako? Mara ngapi umefahamu mtu fulani amefanya nini mwaka huu huku wewe ukiwa hujafahamu umekamilisha nini na huna mpango huo?

Utayafikia mafanikio unayostahili kama utachukua hatua ya kujisoma na kujielewa wewe kwanza badala ya kuhangaika kufuatilia taarifa za watu wengine na nyingi zikiwa hazina mchango kwako.

Unapoanza kujisoma wewe kwanza, mazuri haya yanatokea maishani mwako;

  1. Unapata mtu sahihi wa kukufahamu wewe halisi. Wewe ni wa kipekee, una uwezo wa kipekee, unaweza kufanya mambo makubwa sana. Lakini utafikia hatua hiyo baada ya kujisoma mwenyewe na kujua una kitu gani cha kipekee.
  2. Unakuwa na muda wa kutosha. Unasema huna muda wa kutosha kwa sababu muda wako mwingi unatumia kuwafuatilia wengine. Anza kujifuatilia kabla ya kuwafuatilia wengine.
  3. Utajua ulipo. Ukijisoma wewe kwanza kwa kujiuliza wapi umetoka na sasa uko wapi utagundua kuwa unahitaji kuweka nguvu kubwa ili kufika unakotakiwa kufika
  4. Utapata muda mzuri kwako. Watu wa kuwasoma na kuwafuatilia ni wengi sana, hutaweza kuwamaliza. Muda mzuri unaoupata, tumia kujimaliza wewe kwa kuzidi kupiga hatua kubwa
  5. Utalipwa. Njia pekee ya kulipwa na watu ni kuwapa thamani. Utafanikiwa kuwa thamani kama utajisoma na kujielewa.

Ndugu! Kuna mambo mengi ambayo umekuwa ukienda uelekeo usiyo sahihi na umekupoteza, unahitaji kugeukia uelekeo sahihi. Utafanyaje?

Kwa kuwa tunakujali, AMSHAUWEZO Consultants imekuandalia semina yenye kichwa PIGA U-TURN 101 ZA MAISHA YAKO. Hii ni semina inayokuwezesha kubadili mwelekeo wa hatua zisizosahihi unazochukua ili kupata mafanikio unayostahili.

Kwa kushiriki semina hii utatambua maeneo kumi ya maisha ambayo umepotea kisha kugeukia uelekeo sahihi na kuanza kupata matokeo ya utofauti kabisa.
Maeneo hayo ni ;

  1. Binafsi,
  2. Fedha/Utajiri
  3. Nidhamu
  4. Mahusiano/Jamii
  5. Kazi
  6. Uwekezaji
  7. Biashara
  8. Fikra
  9. Afya

Mpaka mwisho wa semina utakuwa umejifunza U- TURNS 101 kwenye maeneo tofauti ya maisha. Pata picha umegeuka mara 101 na kuelekea upande sahihi, hakika utaboresha maisha yako sana.

Semina hii itafanyika kwa njia ya kundi maalumu la wasap kuanzia Julai 20 – 29,2023.

Ada ya semina hii ni sh 10,000/ ambayo unalipia kupitia mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika).

Utajisikiaje ndugu kwa sh 10,000/ h unapata mambo 101 ya kuboresha maisha yako kwenye maeneo 10 muhimu? Naamini unajisikia vizuri na kupendelewa.

Zimebaki siku 10 tu!

Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii, jiunge leo kwenye kundi hili la wasap kwa kubonyeza kiunganishi hiki https://chat.whatsapp.com/Lmel6ehEr30K5a1S1BCEYu

Karibu sana.

Kwa maelezo wasilana

Mwl. Alfred Mwanyika
0752 206 899
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *