Hukui Kwa sababu Umeiga Kiburi cha mlima.


Categories :

Naamini utakuwa bado unakumbuka somo la jiogorafia kuwa mlima mrefu zaidi duniani ni mlima Everest uliopanda mita 8,848 kutoka usawa wa bahari.

Pia nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kuwa na mlima mrefu zaidi katika bara la Afrika wenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.

Lakini licha ya milima hii kuwa mirefu kiasi hicho cha ajabu ni kuwa haiajawahi kuongezeka hata kidogo. Miaka nenda miaka rudi imebakia vile vile.

Lakini milima hii imeendelea kuvimba na kuiishinda mingine kwa sababu ya hata milima hiyo mingine haikui.

Lakini wewe ulipoiiga milima hii umeumia na hii ndiyo sababu kubwa iliyokufanya kuendelea kubaki ulipo kama sio kuporomoka kabisa.

Baada ya kupata mafanikio fulani ulivimba sana na kujiona umefika mwisho na huhitaji kuweka jitihada zozote tena.

[ ] Hukutaka kujifunza tena kama mwanzo hii imesababisha upitwe na wakati.

[ ] Hukuweka jitihada za kukua hivyo sasa unakufa. Hukutafuta wateja wapya ili waongeze mauzo, biashara yako inakufa.

[ ] Uliwadharau wengine kwa sababu uliona wapo chini yako na hawana thamani kwako. Ulisahau hao ndiyo waliokupa mafanikio yako ya sasa. Sasa wamekuacha ndiyo unaona umuhimu wao.

Lakini jambo la pili ulilouiga mlima na limekugharimu ni hili; Mlima ulipojilinganisha na milima mingine au vichuguu, wewe uliamua kujilinganisha na watu wengine. Kwa sababu wapo chini yako umejifariji kwa kujiona upo juu sana kumbe siyo kipimo sahihi.

Kwa kujilinganisha na watu wengine umeshindwa kuamsha nguvu kubwa zaidi iliyopo ndani mwako ya kufanya mambo makubwa zaidi.

Chukua Hatua;

  1. Acha kuvimba kwa sababu ya mafanikio uliyoyapata, ni kidogo kuliko unachostahili. Nyenyekea, jifunze zaidi, tumia mafaniko haya kama mtaji wa kufanya makubwa zaidi.
  2. Acha kujilinganisha na mtu mwingine yoyote isipokuwa kuwa wewe mwenyewe.
    Angalia uwezo wa kipekee ulionao kisha kila wakati uangalie, ni kwa kiasi gani umeshatumia. Kwa kuwa bado una uwezo mkubwa ndani yake Anza kuuamsha kwa kuweka malengo makubwa zaidi ya sasa. Jisukume kuyatimiza.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *