Utafanikiwa Kama Utakubali Kufa Kwanza.


Categories :

Kufa tena! Inawezekana ni kauli iliyokushitua sana kuwa maisha yako yatakuja baada ya wewe kufa. Ni kweli kifo kinaogofya lakini kuna vifo vinavyoleta uhai.

Ili mbegu iliyofukiwa chini kwenye ubichi iweze kuota maganda yake lazima yaoze kwanza ndipo mbegu hiyo. Maganda yasipokubali kufa hakuna kinachoota.

Tofari bichi hupata uhai baada ya kuuliwa na moto kwanza kwa muda mrefu. Ndipo huwa hai kwa kuwa imara usioweza kuvunjwa kirahisi.

Kisu hupata uhai wake kwa kukubali kinoleo kupita juu yake. Ndipo kisu hicho huwa kikali sana.

Rafiki yangu! Hata wewe unahitaji kufa kwanza ili uwe na uhai wa maisha yako. Huku siyo kufa na kuingizwa kwenye jeneza bali kufa katika tabia za zamani.

Una tabia ulizonazo zilizo hai na zimeua mafanikio yako. Hizi baadhi ya tabia zilizoua mafanikio yako;

[ ] Kutokuja nini unahitaji na hivyo kuamua kufanya chochote.

[ ] Kutokuweka malengo na hivyo kwenda uelekeo wowote ule.

[ ] Kuwa mvivu ukifikiri vitu vinaweza kutokea bila kuweka kazi.

[ ] Kushugulika na maisha ya wengine huku ya kwako ukiyatelekeza.

[ ] Kutokutoa thamani kwanza kwa watu wengine ukitarajia kuwa fedha zitakujia hivi hivi.

[ ] Kutumia zaidi ya kipato chako hivyo kiishia kukopa mikopo mibaya.

[ ] Kutumia fedha yote inayopita kwenye mikono yako bila ya kuweka akiba yoyote.

Tabia hizi zinahitaji kuuliwa ili maisha yako yachipue. Unaziua tabia hizi kwa kuanza kubadili mtazamo wako kwanza kisha kuweka tabia mpya.

[ ] Ua kufanya chochote fanya maalumu .

[ ] Ua kwenda kokote, weka malengo.

[ ] Ua uvivu penda kazi.

[ ] Ua kushughulika na maisha ya wengine, shughulika na ya kwako.

[ ] Ua kutumia zaidi ya kipato, tumia chini ya kipato chako.

[ ] Ua kutoweka akiba, weka 10% ya kila kipato chako.

Tabia gani imesababisha kushindwa kwako? Basi anza kuua tabia hizo hapo na nyingine zinazofanana na hizo.

Leo unaanza kuiua ipi?

Kipate kitabu chako cha JENGA NIDHAMU KALI ili uweze kuua tabia za zamani kisha kujenga tabia ya nidhamu kali itakayofufua maeneo mengi ya maisha yako ambayo yamekufa. Wasiliana 0752 206 899 kukipata kitabu hiki.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *