Ziige Tabia 12 Za Waliofanikiwa Sana(Sehemu ya Kwanza).


Categories :

Kama kuna watu wanaofanikiwa sana huku wengine wakishindwa sana basi pia kutakuwa na kitu kinachowatofautisha sana hao waliofanikiwa na walioshindwa.

Kitu hicho ni TABIA. Waliofanikiwa na vitu wanavyovifanya kila wakati kama sehemu yao ya maisha ambavyo ni tofauti na walioshindwa.

Kwenye makala hii utajifunza tabia 4 kati ya 12 ambazo watu waliofanikiwa wanaziishi na walioshindwa hawazaiishi. Habari njema ni kuwa hata wewe mwenyewe ukizijenga tabia hizi lazima utafanikiwa.

  1. Wanachagua nidhamu na siyo hamasa.
    Waliofanikiwa hawasubiri mpaka wahamasishwe ndiyo wachukue hatua, bali wanajenga tabia ya nidhamu. Wanajenga nidhamu kali ambayo inawafanya wanajisukuma kuchuka hatua hata pale ambapo hawajisikii.
  2. Wana malengo ya wazi kabisa.
    Waliofanikiwa hawaamki asubuhi na kwenda kufanya chochote, bali wanaweka malengo ya wazi kabisa ya nini wanataka kukifanya na kwa wakati gani.
    Kupitia kuweka malengo wanaelekeza nguvu, muda, fedha na uzingativu sehemu moja na hivyo kuwa na uzalishaji mkubwa.
  3. Wanajua kinachoendelea kwenye maisha yao.
    Wanajifanyia tathmini mara kwa mara ili kujua mwenendo wa utekelezaji wa malengo yao.
    Kila siku kabla ya kulala, wanajifanyia tathmini juu ya majukumu waliyopanga kufanya asubuhi yake.
    Lakini wanafanya hivyo pia kila wiki, mwezi au miezi mitatu…
  4. Wanachukua hatari zilizopimwa.
    Ili kuweza kupata matokeo ambayo hawajawahi kuyapata, wanafanya vitu ambavyo hawajawahi kuvifanya. Lakini hawaendi “kichwakichwa” bali wanaainisha kila hatua watakayochukua na hatari wanazoweza kukutana nazo kisha kuwa tayari kulipa gharama. Chukua hatua:
  5. Weka lengo lilowazi kabisa unalotaka kulikamilisha. Je ni kuongeza kipato chako mara mbili?
  6. Ainisha nidhamu unazotakiwa kujenga ili kuweza kulifikia lengo hilo. Je ni kuwahi kuamka? Kujifunza kila siku? Au kuweka 10% ya kila kipato chako?
  7. Ainisha hatari unazotakiwa kuzichukua ili kupata matokeo ambayo hujawahi kuyapata. Je ni kuanza biashara mpya?
  8. Jifanyie tathmini kila siku. Ona ni kwa kiasi gani unafanyia kazi lengo lako; ainisha na fanyia kazi changamoto zako.

Kila la kheri.

Jipatie kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ili kikusaidie kujenga tabia muhimu ya mafanikio; NIDHAMU badala ya kutegemea hamasa ambayo huisha angali ndiyo unaanza safari. Wasiliana 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *