Tabia 12 Za Waliofanikiwa Sana(Sehemu ya Pili).


Categories :

Kama kuna watu wanaofanikiwa sana huku wengine wakishindwa sana basi pia kutakuwa na kitu kinachowatofautisha sana hao waliofanikiwa na walioshindwa.

Kitu hicho ni TABIA. Waliofanikiwa wana vitu wanavyovifanya kila wakati kama sehemu yao ya maisha ambavyo ni tofauti na walioshindwa.

Kwenye makala iliyopita ulijifunza tabia 4 za kwanza kati ya 12 ambazo waliofanikiwa wanaziisi na kuwa sababu ya kufanikiwa kwao. Karibu kwenye sehemu ya pili ya tabia za waliofanikwa. Leo utajifunza tabia ya 5 mpaka ya 8;

  1. Wanafanya vichache kwa ubora. Waliofanikiwa wanatambua kuwa kufanikiwa siyo jambo la kufanya vitu vingi kwa pamoja kwa kugusagusa tu bali vichache lakini kwa ubora zaidi.

Wanachagua biashara moja kwanza na kuijenga mpaka inakuwa kubwa kabla hawajaanzisha nyingine. Wanajua kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja ni kutawanya nguvu, muda, umakini na rasilimali na hivyo kuishia kuwa na ufanisi mdogo.

  1. Wanapangilia vizuri na kutafsiri mambo.
    Waliofanikiwa wanahakikisha kila kitu kinapangiliwa vizuri. Wanapangilia majukumu ya siku, na kurekodi matokeo wanayoyapata huku wakitambua maana ya matokeo hayo.

Hii inwasaidia kujua mwenendo wa vile wanavyovifanya kisha kutoa nafasi ya kufanya marekebisho pale inapotakiwa.

  1. Wanatengeneza mtandao wenye faida.
    Waliofanikiwa wanatambua kuwa ili ufanikiwe unahitaji kuwa na mtandao wa watu wenye faida kwenye jitihada mipango yako. Hivyo wanajihusisha na watu sahihi ili wawasaidie kufikia malengo yao.

Hawajihusishi na watu tu kwa sababu wapo bali wanakuwa makini nani wajiunge nao.

  1. Wanajifunza kila wakati.

Waliofanikiwa wanatambua kuwa hakuna namna yoyote ambayo utayatenga mafaniko makubwa na maarifa. Kwa kuwa wanataka kuchukua hatua mpya na kwa usahihi, wanahakikisha wanajifunza vitu vipya kila wakati na kuvitumia.

Ndugu! Habari njema ni kuwa na wewe unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kama utajenga tabia hizi ambazo waliofanikiwa wamezijenga. Chukua hatua sasa.

Chukua hatua:

  1. Kwenye biashara nyingi unazozifikiria ua ulizonazo chagua moja kisha weka nguvu zako zote, umakini, muda…..uvumilivu kwenye biashara hiyo moja mpaka isimame na kuwa imara kabla hujaenda kuanzisha nyingine.
  2. Orodhesha watu uliotengeneza mtandao nao kisha tathmini ni kwa kiasi gani wanakusaidia kutimiza malengo yako. Jitenge na wale wanaokurudisha nyuma kisha jiimarishe na wale waliosahihi.
  3. Weka kipaombele kwenye kujifunza. Kwa kuwa nguvu kubwa ya mafunzo ipo kwenye vitabu; chagua kwenye orodha hapa chini kitabu utakachoanza kukisoma sasa ili kikusaidie kupiga hatua kubwa zaidi. *1. AMSHA UWEZO WAKO HALISI
  4. DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO
  5. UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA
  6. JENGA NIDHAMU KALI*

Wasiliana kupitia 0752 206 899 ili kujipatia vitabu hivi sasa.

Kila la kheri.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *