Hii Ndiyo Mizimu Itakayosimama Mbele Yako Dakika Chache Kabla Ya Kufa…..


Categories :

Kama una uhakika ulizaliwa basi naamini utakuwa na uhakika kama utakufa. Uhakika huo unao kwa sababu kuna waliozaliwa umewashuhudia wakifa.

Kama kuna kitu unachotakiwa ujivunie na kushukuru sana ni kuwa hai mpaka siku ya leo. Na kama kuna swali unalotakiwa ujiulize mara kwa mara wakati wa uhai wako ni kwa nini upo hapa duniani?

Katika uhai ulionao kuna vitu vinavyokujia ambavyo unatamani uwe navyo au uvifanye. Lakini pia kuna maeneo unatamani ufike. Kuna nafasi ya uongozi ambayo nafsi yako inakuambia hiyo ni yako.

Mtu wako wa ndani hajatulia akikukumbusha mara kwa mara lakini wewe hujazingatia au kujisukuma kuchukua hatua. Leo nakukumbusha kuwa mambo haya ndiyo yatakayosimama mbele yako muda mfupi kabla hujafa. Hii ndiyo mizimu itakayokuwa inakukumbusha kuwa ulitakiwa unitekeleze lakini hukufanya hivyo.

  1. Biashara uliyotakiwa kuijenga.
    Unatambua wazi kabisa kuwa biashara ndiyo njia pekee ya kukupa kipato kikubwa cha kukupa utajiri. Umekuwa ukipata wazo nzuri la biashara lakini huanzishi biashara hiyo unasema utaanzisha kesho. Inawezekana umeianzisha lakini hujaiwekea nguvu kuikuza. Huu ni mzimu utakaosimama unapotaka kufa ukikuuliza kwa nini hukunianzisha na ukawa na kipato kikubwa?
  2. Nguvu kubwa ambayo hujaitumia.
    Kama mafanikio ya dunia yaliyopatikana sasa duniani yametokana na 10% ya uwezo wa mwanadamu, basi usipouamsha wa kwako kwa kuwa na ndoto kubwa basi kuna uwezekano wa zaidi ya 90% ya uwezo wako ukawa unakutazama kama mzimu dakika chache kabla hujafa.

Je utakuwa ni mawazo ya thamani kubwa ambayo hukuyafanyia kazi? Je zitakuwa ni nguvu nyingi za mwili unazotaka kufa nazo ambazo hukuzitumia kufanyia kazi kubwa?

  1. Utajiri ambao ungeupata kwa kutoa thamani kwa wengine.

Una uwezo wa kuwa tajiri na utajiri wako upo kwenye thamani unayoweza kutoa kwa wengine kupitia huduma au bidhaa. Usipojisukuma kutoa thamani kubwa zaidi kwa watu wengine utajiri huo unaendelea kubaki ndani yako. Kumbuka hii ndiyo thamani ya utajiri itakayosimama mbele yako ikikushitaki kwa nini hukunipeleka kwa watu!

  1. Alama ambayo hujaiweka duniani.
    Kwa upekee ulionao unatakiwa uiachie dunia alama kwa kugusa maisha ya watu na kuwa kumbukumbu isiyofutika. Je ni uongozi uliotukuka? Uvumbuzi ilioufanya? Kama utakuwa unakufa ingali alama hiyo hujaiacha kwa watu, basi kumbuka itakuja mbele zako ikikushitaki.
  2. Kusudi ambalo hukulitimiza.
    Upo hapa duniani kwa sababu maalumu yaani kutatua tatizo maalumu. Je umeshatambua kusudi lako na kuanza kuliishi? Kama hapana basi kumbuka dakika chache kabla ya kufa kitu ambacho kilikuwa kinakuudhi sana na ukawa unaona unaweza kutatua kitasimama mbele yako kama mzimu ukikushitaki.

Je mzima gani ukifa sasa utakuwa unakushitaki?

Habari njema ni kuwa kama bado upo hai una nafasi ya kufuta mashitaka ya mizimu yote hii kwa kuamsha uwezo wako na kufanya mambo makubwa yatakayotimiza sababu ya wewe kuwepo hapa duniani.

Jipatie kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ili kikuongoze namna ya kutoa thamani kubwa kipindi cha uhai wako na kutoacha deni lolote hapa duniani. Wasiliana 0752 206 899 kujipatia kitabu hiki sasa.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *