UWEZO NA BIASHARA – 01.


Categories :

Ndani yako kuna nguvu kubwa ambayo bado haijatumika. Nguvu hiyo inaitwa UWEZO.

Nguvu hizo zipo kwenye akili(mawazo/mtazamo), mwili, roho & hisia.

Licha ya mafanikio makubwa ambayo dunia imepata kwa mfano teknolojia, usafiri wa anga na maji, matibabu, miondombinu….lakini binadamu ametumia wasatani wa 10% ya uwezo wake.

Je kama aliyegundua ndege ametumia 10% ya uwezo wake, wewe utakuwa umetumia %?. Je ni 0.00000….1%? Jibu unalo mwenyewe.

Habari njema ni kuwa kama bado upo hai una nafasi ya kutumia nguvu hiyo kufanya makubwa kabla hujafa.

Moja ya sehemu unayoweza kutumia uwezo huu ni kwenye kujenga utajiri, yaani uhuru wa fedha. Kwa nini utajiri? Kwa sababu ukiwa na fedha nyingi utaweza kutatua changamoto zako nyingi.

Lakini njia ya uhakika ya kupata utajiri ni kuwa na biashara yanye mafanikio. Hii ni biashara inayotengeneza faida kubwa na inayoweza kujiendesha.

Kumbe unaweza kuanza kuamsha uwezo wako ulionao ndani yako kwa kuanza;

Kufikiri biashara unayoweza kuifanya. Kwa kuanzia, angalia changamoto ambazo zinaikumba jamii inayokuzunguka kisha njoo na sululisho, ukianza kutatua changamoto hizo, watu watakuwa radhi kulipia bidhaa au huduma unayoitoa.

AU

Kama tayari una biashara, amsha uwezo wako ili kuikuza biashara yako. Jisukume kuwahudumia wateja wako kwa ubora zaidi, wafikie wateja wengi zaidi, weka malengo makubwa zaidi kwenye biashara yako na jisukume kuyafikia. Ndipo biashara yako itakapokua sana na kukupa utajiri.

Anza sasa kunufaika na nguvu hii iliyopo ndani yako tangu kuzaliwa kwako kwa kuanzisha na/au kukuza biashara yako.

Chukua hatua.

  1. Chunguza na tafakari mazingira yanayokuzunguka. Je kuna changamoto gani ambayo wewe unaweza kuanza kuzitatua? Anzia hapo kupata wazo la biashara yako.
  2. Kama tayari una biashara, ainisha mauzo yako ya sasa kwa wiki au mwezi kisha zidisha mara mbili. Hilo liwe lengo lako la kuanzia kukuza mauzo. Fanya mara mbili kwenye yale yote uliyokuwa unafanya mwanzoni. Wafikie wateja mara mbili zaidi; watembelee, wapigie simu, omba rufaa kwa wateja wanoakuja kununua kwako.

Kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA kimeeleza kwa kina hatua kwa hatua namna unavyoweza kuamsha uwezo wako kisha kupata wazo la biashara pia kukuza biashara uliyonayo. Kupata nakala hii wasiliana nami sasa kupitia 0752 206 899.

Karibu sana.

Imeandikwa na;
Alfred Mwanyika,
AmshaUwezo Consultants,
“Pata Unachostahili”
0752 206 899

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *