Unateseka Bure…Unachokihofia hakipo !


Categories :

Mtu alikuwa anapita kwa woga usiku kwenye njia aliyopita mchana, ghafla taa ikawashwa kwenye nyumba ya karibu na kulikuwa hakuna kitu cha hatari kilichokuwepo. Akajiuliza moyoni nilikuwa naogopa nini?

Baada ya kuambiwa mto anaokwenda kuvuka kesho una mamba, hakulala usingizi huku akiwaza atavuka vipi. Alipofika kwenye mto huo akaona kuna daraja la kuvukia ambalo hata kama mamba akiamua kumrukia hawezi kumfikia, akajilaumu sana kwa nini hakulala usingizi usiku.

Baada ya kuwa unatembea usiku kwenye mwanga, ghafla ukaona kama kuna mtu anakufuata kwa nyuma,  baada ya kuchunguza vizuri ukaona kumbe ni kivuli chako! Ukavuta pumzi na moyo wako ukatulia.

Ulipokuwa mtoto ulikubali kurushwa juu na kuachiwa huku ukifurahi kwa sababu uliamini utadakwa tena. Vipi mtu akisema akurushe hivyo leo?

Siku ya kwanza kuanza kujifunza baiskeli,  jasho lilikuwa linatoka mpaka kwenye meno huku akili yako ikiona unataka kudondoka lakini sasa ukiwa unaendesha akili yako ikiona unaongeza kasi. Jifunze kitu hapo.

Ndugu! Kuna mambo mengi uliyoyahofia yakakuumiza lakini hayakutokea, na hata pale yalipotokea maumivu yake hayakuwa makali kama yale uliyodhania na kuumia.

Kuna biashara umekuwa ukiahirisha kuanzisha  kwa kuhofia kupata hasara lakini hujafanya ukathibitisha hilo!

Kuna mtu umeshindwa kumwendea akupe msaada ambao ungekusaidia kupiga hatua kubwa, lakini hujafanya hivyo ukiogopa kuwa utakataliwa.

Hofu ni kitu ambacho katika uhalisia hakipo lakini unakitengeneza mwenyewe akilini mwako.

Hii imekuchelewesha sana kwenye safari yako ya mafanikio. Anza kuchukua hatua muhimu sasa ulizozihofia kwa muda mrefu.

  1. Anzisha biashara uliyoihofia kwa muda mrefu.
  2. Nenda kamuone mtu muhimu anayeweza kukupa msaada wa kupiga hatua kubwa.
  3. Kakutane na wateja wakubwa uliowaogopa ambao watakubali na kuanza kununua kwako.

Jipatie kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA ili kuanza kuifanya biashara uliyoihofia siku nyingi. Una nguvu kubwa ya kukabiliana na changamoto inatayokukuta kisha ukasonga mbele.

Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia kitabu hicho sasa kwani nakala za ofa zimebakia chache mno.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952.
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *