Vua Kinyago Chako Ujione Wewe Halisi.


Categories :

Gogo au jiwe ambalo umekuwa ukilipita kila siku litakuwa kinyago kinachopendeza, chenye thamani na kitakachokushangaza baada ya mchongaji kutoa maganda yaliyokuwa yanakizuia.

Mtu akivaa kinyago hubadilika sura kabisa na kuwa kitu kingine. Watu wamekuwa wakivaa vinyago na kuficha uhalisia wao . Hii ni kwa nia njema au mbaya.

Habari mbaya ni kuwa na wewe ni miongoni mwa watu ambao wamevaa vinyago wakaficha uhalisia wao na dunia imeshindwa kuwatambua.

Kuna uwezekano wa kuwa umevaa kinyago bila kujijua. Tumekuwa tukikuangalia na jinsi tunavyokuona si wewe halisi.

Nakushauri kaunzia leo vua vinyago ulivyovaa ili uanze kuonekana wewe halisi.

  1. Vua kinyago cha unyonge. Umekuwa mnyonge mpaka kujidharau. Lakini una nguvu kubwa ndani yako za kufanya mambo makubwa. Vua kinyago cha unyonge kisha weka wazi ujasiri kwa kujiambia na kufanya mambo makubwa.
  2. Vua kinyago cha umasikini. Hali ya kiuchumu uliyonayo ni kwa sababu akili yako imevaa umasikini. Umejiona huwezi kuwa tajiri. Hukuzaliwa kuwa masikini, kuanza kuukataa ni hatua muhimu sana kwenye kuonyesha uhalisia wa utele ulinao maishani mwako.
  3. Vua kinyago cha hofu. Kwa sababu umekubali kuvaa hofu maishani mwako, hakuna hatua mpya unayopiga. Jipe ujasiri leo, unachokihofia hakipo. Anza kufanya yale unayoyahofia ili uanze kupata matokeo halisi.
  4. Vua kinyago cha kukata tamaa. Umekuwa laini sana. Ukianzisha kitu kisha kupata changamoto,  unakata tamaa. Hatuoni matokeo ya mipango yako kwa sababu ya kinyago cha kukata tamaa ulichovaa. Vua kinayago hicho ili tuone uhalisia wa ustahimilivu wako.
  5. Vua kinyago cha mazoea. Unapata matokeo yaleyale kila siku hivyo tunakosa uhasilia wa makubwa unayoweza kuyafanya. Ukivua mazoea yako tutaona uhalisia wa mambo ya utofauti unayoweza kufanya.

Rafiki! Kuna mambo ya tofauti na makubwa unayoweza kufanya kama utakubali kuvua vinyago ulivyovaa sasa.
[  ] Vua unyonge vaa ujasiri
[  ] Vua umasikini vaa utajiri
[  ] Vua hofu chukua hatua
[  ] Vua kukata tamaa vaa uvumilivu
[  ] Vua mazoea vaa utofauti

Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo wa kukusaidia kuvua vinyago vyako kisha kuanza kuamsha nguvu halisi uliyonayo ndani yako kisha kupata mafanikio makubwa unayostahili.

Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako leo kwa bei ya ofa. Chukua  hatua hii muhimu, wasiliana nasi sasa.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *