Usihangaike Huko, Ukubwa Wako Upo Hapa……


Categories :

Kama ukubwa ungeangaliwa kama umbo basi nyuki angesahaulika kabisa kwenye orodha licha ya asali yenye thamani kubwa anayoitengeneza

Je umekuwa ukihangaika sana na kwa muda mrefu kutafuta nini ufanye ili maisha yako yawe na mafaniko makubwa ?

Je umekuwa  ukifanya mjaribio mengi nini ukifanye ili uwe na mchango kwenye dunia hii?

Je umekuwa ukihangaika nini ufanye ili upate ridhiko ndani ya moyo wako?

Je umekuwa ukingaika nini ufanye ili ufe angali dunia haikudai chochote?

Usiwe na wasiwasi leo utajua ni ufanye ili uweze  kuutambua na kuutumis ukubwa wako.

Njia pekee ya kufikia ukubwa wako yaani kuishi maisha ya mafaniko makubwa dunia ni kujua sababu ya uwepo wako hapa duniani na nini uliumbwa nacho.

Kila kitu unachokiona hapa duniani, hata unachokiona hapo ulipo kina sababu yake ya kutengenezwa. Kiti kwa ajili ya kukalia, mimea kutupa chakula na hewa, nyuki kutupa asali tamu sana….

Kadhalika kila binadamu unayemuona ikiwa pamoja na wewe ana sababu maalumu ya kuwepo wake hapa duniani.  Akiitambua sababu hiyo kisha kuiishi, lazima afanye makubwa katika maisha yake.

Katapila linafanya kazi yake vizuri hata kutembea kwenye tope kwa sababu limewekewa nguvu hizo ndani yake. Hata wewe unapotambua sababu yako ya kuwepo hapa duniani inakuwa rahisi kuamsha uwezo wako wa kipekee ndani yako ili kuweza kutimiza sababu yako.

Trekta haliwezi kuanza kushindana kasi na basi, kwani linatambua kufanya hivyo ni kujichosha na kujichelewesha kwenda kulima shamba linalolisubiri.

Umeumbwa ufanye nini? Nini unaweza kukifanya kwa ustadi mkubwa? Haya ni maswali mawili muhimu ya kujiuliza ili uweze kutambua na kuuishi ukuu wako.

Swali la kwanza linakusaidia kujua kusudi la maisha yako na la pili linakusaidia kutambua uwezo wa kipekee ulionao ndani yako wa kufanya makubwa.

Kusudi lako limefichwa kwenye changamoto ambayo kila unapokutana nayo, moyo wako unapata mahangaiko makubwa kwa kuona una wajibu na uwezo wa kuitatua.

Uwezo wako wa kipekee upo kwenye vitu unavyopenda kuvifanya na unavifanya kwa viwango vya juu kiasi cha watu wengine kukushangaa.

Ndugu! Naamini unatamani ufikie ukuu kwenye maisha yako. Anza kwa kujiuliza maswali hayo mawili muhimu hapo juu. Ukipata majibu ya awali, endelea kuyaboresha kwa kuyafanyia kazi mpaka kila kitu kinakuwa wazi kabisa.

Kwa msaada zaidi kuhusu namna ya kufikia ukubwa wako soma kitabu kiitwacho AMSHA UWEZO WAKO HALISI. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako leo.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *