Mchawi Umemtengeneza Mwenyewe……
Nyuki alipokataa kujidharau kwa sababu ya umbo dogo ndipo alipotengeneza asali ambayo imekuwa kielelezo cha utamu duniani.
Kinyonga kilipokataa kujidharau kwa sababu ya kushindwa kutembea haraka ndipo alipoishi na kutuonyesha ufahari wa rangi.
Samaki alipokataa kujidharau kwa sababu tai anamringia kwa kuelea hewani ndipo alipofanikiwa kutafuta na kuyapata maji kisha kuayatawala.
Kuna dhambi umeifanya na inakuhukumu, dhambi hiyo ni kujidharau. Umejiona hufai kisha umepata matokeo ambayo hayafai.
Kwa kuona huwezi kufanya makubwa, umeipuzia hata ndoto inayokuja ndani yako mara kwa mara ya kufanya makubwa. Umeamua kuendelea na mambo yako ya kawaida.
Ulipowaangalia watu wengine na kuona wamefanya makubwa, umejiona hao ndiyo wenye bahati na wewe wa bahati mbaya. Umesahau kuwa wewe ni wa pekee na thamani yako haiwezi kulinganishwa na wengine.
Ulipojaribu kitu mara moja kisha kukosa matokeo, ukajidharau kwa kuona wewe huwezi na waliofanikiwa ndiyo wenye mafanikio. Umesahau kuwa hata hao waliofanikiwa walishindwa sana kabla ya kuwa washindi.
Ulipokumbuka umri wako ukaona hakuna kitu cha maana unachoweza kufanya kwa sasa. Lakini umesahau kuwa kama bado upo hai mpaka leo basi kuna kitu cha thamani unaweza kukifanya vinginevyo ungekuwa umeshakwisha kufa.
Kwa nini umekubali matukio ya kushindwa yahushe thamani yako ya pekee? Wewe ni mtu wa pekee sana katika dunia hii. Dunaia inasubiri kwa hamu kubwa zawadi utakayotoitoa pale utakapoacha kujidharau.
Itubu dhambi hii ya kujionea uliyoifanya kisha jiambie kuwa kuna thamani kubwa sana ipo ndani yangu na ni jukumu langu kuionyesha thamani hii na dunia ikawa tayari kukilipa.
Unaona nini ndani yako? Amini kuwa unaweza na dunia ipo tayari kukuwezesha kama utakuwa na shauku ya kufanya makubwa. Tengeneza ndoto ya kitu kikubwa unachotamani kukifanya katika kipindi cha uhai wako. Weka mipango ya kuanza kutimiza ndoto hata kwa udogo unaoweza kuuanza sasa kisha endelea kukua.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni msaada mkubwa sana kwako wa kuacha kujidharau kisha kuanza kufanya makubwa sasa.
Jipatie nakala yako leo kukomesha dharua zako. Kitabu hiki kinapatikana katika mfumo wa nakala ngumu(hardcopy), tete(softcopy) na sauti (audio). Wasiliana kupitia namba 0752 206 899 kujipatia nakala yako kwa bei ya punguzo. Zimebaki nakala chache sana za bei ya punguzo.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz