Tumia Mbinu Hizi 6 Kukabiliana Na Mdudu Huyu Anayezuia Mafanikio Yako .


Categories :

Kil mtu anatamani kupata mafanikio tene yale makubwa. Kama kuweka malengo kwa ajili ya kuyafikia mafanikio hayo wengi wameyaweka. Lakini ukiuliza ni wangapi wameyapata mafanikio hayo, ni wachache sana.

Watu wana malengo mikononi. Lakini wanaendelea kubakia nayo bila ya kufanyia kazi. Moja ya kikwazo kikubwa cha watu kutofanyia kazi malengo yao ni mdudu anayeitwa KUAHIRISHA.

Ni mara ngapi umepanga kuanza kitu lakini huanzishi? Ni mara ngapi umepanga kabisa kuanza kuboresha ufanyaji wako wa mambo, lakini kila siku unasema kesho? Ni mara ngapi umeweka lengo la kuacha tabia fulani mbaya lakini muda ukifika unasema kesho!

Hakuna matokeo yoyote unayoweza kuyapata bila ya kufanya kitu hicho. Lakini pia huwezi kufanya kitu kama utaendelea kuahirisha. Kazi inatangulia matokeo, ndiyo maana kwa sababu ya kuendelea kuahirisha kwako, umeendelea kubaki hapo hapo.

Zifuatazo ni mbinu 8 unazoweza kuzitumia ili kukabiliana na mdudu huyu kuahirisha kisha ukaanza kupata matokeo.

1. Gawa lengo kubwa kwenye vipande. Moja ya sababu inayokufanya uone uvivu kuchukua hatua ni kuona una kazi kubwa sana mbele yako. Baada ya kuwa na lengo kubwa la mwaka, ligawe kwenye vipande vya kila mwezi, wiki, juma, siku na baadaye saa. Lengo la saa litakuwa dogo na hivyo kukuhamasisha kuchukua hatua.
Kama unataka kuingiza kipato cha sh milioni 10  kwa mwaka, gawa lengo hilo kuwa wastani sh 835,000/ kwa mwezi, wastani sh 210,000/ kwa wiki, wastani sh 30,000/ kwa siku. Hivyo unapoamka asubuhi unajua unaenda kutafuata kipato cha sh 30,000/. Hii inakuahamasisha kuliko kusema unaenda kutafuta sh milioni 10.

2. Weka mwisho wa lengo (deadline). Msukumo wa mtu kuchukua hatua huamka pale anapoona muda wa mwisho umekaribia. Hivyo kwenye kila kazi unayotaka kufanya weka deadline.

3. Kaa mbali na usumbufu. Katika zama hizi kuna usumbufu mwingi unaokuhamasisha kuahirisha kile ulichokipanga kufanya. Usumbufu mkubwa uliopo sasa ni simu yako. Kama kazi unayoifanya haihusishi simu, basi iweke mbali na wewe wakati unafanya kazi hiyo. Kama kazi yako inahitaji simu, basi funga programu nyingine usizozitumia kwenye kazi hiyo.

4.  Weka vipambele. Kuna kazi nyingi zinazoibuka mbele yako kila wakati. Ili ufanye zile zenye maana basi pangilia kazi za kufanya siku hiyo kulingana na vipaombele na anza na zile zilizopo juu ya orodha.

5. Jipe motisha. Pale unapofanikiwa kukamilisha kazi, hata kama ndogo jipongeze hata kwa kujipigia makofi ana kufanya kile unachokipenda. Hii itakuhamasisha kuendelea na kazi inayofuata.

6. Jenga nidhamu. Yafanye yale unayotakiwa kufanya kama tabia yako. Kila unapopanga kufanya kitu, jisukume kufanya. Ukirudia hivyo kwa msimamo na muda mrefu, itakuwa ni sehemu ya maisha yako.

Ndugu! Mafanikio yataanza kukufuata baada ya kumuondoa mdudu huyu katika maisha yako. Kabiliana kwa uhakika kwa kujijengea nidhamu kali katika maisha yako. Hii ni nidhamu ya kujisukuma kuchukua hatua hata pale unapokuwa hujisikii au kuona kuna sababu ya kutofanya.
Ili kujenga nidhamu hii kali hakikisha unakipata kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI. Huu ni mwongozo wa kukufanya uwe unatoa MATOKEO na siyo SABABU kwenye maisha yako. Kuwa miongoni mwa watu wachache watakaopata nakala ya Kitabu hiki kwa bei ya ofa ,sh 14,999/ badala ya sh 20,000/. Wasiliana sasa kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala hiyo ili uanze kupata matokeo uliyoyakosa kwa muda mrefu sasa.

Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *