Siri 5 Zitakazokupa Maisha Ya Uhuru Na Mafanikio Makubwa.
Picha hii ilete mapinduzi makubwa katika maisha yako. Jifunze siri tano kutoka kwenye picha hiyo;
- Maisha yako ni muda na muda ndiyo maisha. Kuna mwanzo na mwisho. Kama leo upo hai basi kuna siku utaondoka. Utumie vizuri muda wako.
- Kanuni ya kuendelea kuishi ni kuendelea kukua. Ukiacha kukua unakufa. Hakikisha kila wakati unakuza kitu, tabia njema, mtaji, biashara, kipato, mahusiano,….
- Usiache kuishi maisha yako kwa sababu ya binadamu fulani, hata yeye atakauka. Usiruhusu kitu chochote kikatishe ndoto yako. Kwani hakuna kinachodumu milele.
- Maisha yako yana majira tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na maumivu, lakini hayatadumu. Hakikisha majira yoyote yale yanakuacha salama na ukiwa umekua.
- Tumia vizuri sana zawadi ya uwezo ulionao kwani kuna siku utatamani uutumie lakini hutaweza.
Soma tena pointi hizi tano huku ukizitafakari kwa kina. Kila utakapovuta pumzi kumbuka kuwa hakuna kitu ulichonacho kitakachodumu milele.
Kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO kitakufanya kuiishi kila siku kwa mafanikio makubwa. Utasoma dondoo 1 kila siku kwa mwaka mzima bila kurudia hata siku moja.
Dondoo hizi zinakusaidia kujenga nguzo 12 za mafanikio ; Uwezo, malengo, kazi, nidhamu, ustahimilivu, fedha, thamani….
Wasiliana nasi 0752 206 899 kujipatia nakala yako.
“Unastahili Zaidi Ya Ulichokipata”
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz