Usife Ungali Hai!


Categories :

Kuna hali ambazo ulipitia, unapitia au unazo zinazokufanya uone maisha yako yamefika mwisho. Unaona kama umeshakufa wakati bado upo hai.

Huku ni kukata tamaa ukiona kuwa hakuna kitu kingine unachoweza kufanya na kupata matokeo ya utofauti.

Ni kama imefika hatua unaona unasubiri kufa katika mazingira tofauti ya maisha; kipato, kazi, afya, mahusiano, kiroho nk.

[  ] Wewe siyo kilema. Kama akili yako inaweza kusoma na kutafakari maana yake; wewe siyo kilema na usijiumbie ukilema. Kuna kitu unaweza kukifanya kwa ajili ya dunia hii, ni kipi hicho? jiulize ndani yako.

[  ] Biashara unayoifanya haitakufa kama wewe hutakubali kufa. Anza kurejesha uhai wako kwanza kwenye biashara hiyo nayo itaanza kuchipua tena. Jifunze zaidi kupitia makosa, hudumia kwa utofauti, wafikie wateja wengi zaidi, usitumie zaidi ya bajeti.

[  ] Acha kulalamika.  Ndugu hakuna kitu kinachoweza kutokea maishani mwako na ukakosa mtu wa kumlalamikia. Badala ya wewe kulalamika kwenye hali yako ya sasa, wewe chukua jukumu la kufanya chochote kilichosahihi.  Hakuna mafanikio kwenye kulalamika.

[  ] Rekebisha mtazamo wako. Matatizo mengi uliyonayo yameanzia kwenye mtazamo wako. Epuka mitazamo hasi. Iishi mitazamo chanya.
     Jione unaweza, ona fursa kwenye changamoto, ona uwezekano hata pale matokeo yanapochelewa.

[  ] Anza hata kwa udogo. Una nafasi ya kuanza kitu kipya kitakachobadili maisha yako, hata kwa udogo wake. Una nafasi ya kuboresha kwa kuanza kidogo kidogo. Usione shida kuanzia chini tena, kumbuka sasa tayari una uzoefu kutokana na changamoto ulizopitia. Hivyo una nafasi ya kukua kwa haraka.

Ndugu! Haijawa mwisho mpaka imekuwa mwisho. Kama bado upo hai una uwezo wa kubadili chochote unachotamani. Una nafasi hiyo, na mabadiliko yenye mafanikio lazima yaanzie akilini kisha kwenye kazi.

Iambie akili yako kuwa unaweza kurudi tena kwenye mstari na kwa nguvu kubwa kuliko mwanzo. Usikate tamaa ungali hai.

Jiulize sasa kuna kitu gani unaweza kukifanya ili kufufua kitu unachokiona kina hali mbaya au kimekufa? Ukianza kuorodhesha utapata majibu mengi tu.
ANZA LEO ANZA SASA ANZA NA ULICHONACHO.

Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo wa kukuwezesha kufufua mambo unayoyaona yamekufa. Kitakusaidia kuamsha nguvu kubwa ambayo imelala tu ndani yako kisha kuitumia kwenye kufufua vitu vyako vilivyokufa.

Kuwa miongoni mwa wachache watakaopata nakala chache za ofa zilizobaki.  Wasiliana sasa kupitia 0752 206 899. Karibu sana.

“Unastahili Zaidi Ya Ulichokipata”

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *