Vitu Vitatu Vya Kukupa Mafanikio.
Mafanikio ni ndoto ya watu wengi, lakini mafanikio ni ndoto isiyotimia kwa watu wengi.
Wapo ambao wameweka nguvu kubwa sana wakitafuta mafanikio, lakini wameishia kuambulia kiduchu. Kumbe kuna viungo vingine vinavyokuwa vinakosekana.
Katika mafaniko yoyote yale unayoyataka, kuna vitu vitatu ambavyo ukiviunganisha pamoja vitakupa mafanikio.
Vitu hivyo ni; unachokifanya, unafanya na nani, na kazi kubwa.
1. Unachokifanya. Hiki ni kitu kinachobeba eneo kubwa la mafanikio yako. Ili nguvu zako utakazoweka wewe ziwe na faida, lazima utambue kitu sahihi kwako kitakachokupa mafanikio. Si kila kitu kitakufaa wewe.
[ ] Chagua kitu unachokipenda kukifanya.
[ ] Unachokifanya kihusiane na uwezo wako wa kipekee.
[ ] Kiwe ndiyo ndoto yako kubwa.
[ ] Kifanye kwa msimamo.
2. Watu wa kufanya nao kazi.
Hakuna mafanikio makubwa unayoweza kuyapata pekeyako. Hata kama utakuwa na nguvu kiasi gani, utapata ukomo kwenye nguvu hizo, muda, maarifa na ujuzi. Unahitaji watu sahihi wa kukusaidia.
[ ] Timu nzuri ya mauzo.
[ ] Washauri na wasimamizi wazuri.
[ ] Watu wenye taaluma nzuri juu ya biashara yako.
[ ] Mahusiano mazuri wa watu wako.
3. Kazi kubwa. Baada ya kuwa na uelekeo sahihi kwa kutambua kipi kitakupa mafanikio makubwa maishani na kuwa na watu sahihi kinachobaki sasa ni kuweka kazi.
[ ] Fanyia kile ulichopanga.
[ ] Kazi kubwa ndiyo inalipa zaidi.
[ ] Jenga urafiki na kazi, ni rafiki asiyeweza kukusaliti ukimfuata.
[ ] Weka umakini mkubwa wakati wa kazi.
Ndugu! Hivi ndiyo viungo vitatu vya mafanikio yoyote makubwa unayoyataka.
Chukua hatua;
- Jiulize ni nini hasa unatamani ukipate maishani mwako? Weka wazi kabisa kwa kuandika. Kumbuka hapa unatengeneza uelekeo sahihi wa nguvu zako.
- Kulingana na kitu sahihi unachotaka kukifanya, tafuta watu sahihi watakaokusaidia kufanikisha lengo hilo kubwa.
- Anza kuweka kazi kubwa. Kwa sababu utakuwa upo kwenye njia sahihi, basi kuweka kazi kubwa kutakupeleka kwenye mafanikio makubwa.
ANZA LEO ANZA SASA ANZA NA ULICHONACHO.
Kutambua biashara sahihi inayokufaa wewe na kukupa mafanikio makubwa hakikisha umejipatia kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA. Huu ni mwongozo utakaokuwezesha kuanza biashara chini kabisa kisha kuikuza na kufikia mafanikio makubwa.
Kuwa miongoni mwa watu wachache watakaozipata nakala chache za ofa zilizobaki. Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899.
“Unastahili Zaidi Ya Ulichokipata”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz