Kumbe Huo Sio Mwisho Wako!


Categories :

Mtafiti mmoja kutoka Chuo Kikuuu cha Harvard alifanya jaribio kujua ni kwa muda gani panya anaweza kuogelea na kustahimili bila kufa?

Ilikuwa inafahamika kuwa kwa kawaida panya huchukua dakika 15 kujitahidi kujiokoa kwenye maji kabla hajachoka na kufa.

Kwenye jaribio hili aliamua kufanya kwa utofauti kidogo. Alichukua panya kadhaa kisha kuwaweka  kwenye glasi iliyokuwa imejazwa maji nusu yake.

Dakika chache kabla hawajazama, aliwatoa panya wale nje ya maji, akawakausha na kuwaacha kupumzika kwa muda. Kisha aliwarudisha tena kwenye maji kwa ajili ya mzunguko wa pili. Je unafikiri walistahimili kwa muda gani kabla ya kufa?
Je dakika 5, 10, 15, 30 au 60?

Itakushangaza! Iliwachukua masaa 60 kuchoka na kisha kufa kinyume na ilivyozoeleka.

Kama wangepata bahati ya kuwauliza panga hao kabla ya kufa nini kilichowafanya walistahimili kwa muda mrefu kiasi hicho? Wangeweza kuwajibu kuwa “Tuliamini kuna mtu angekuja kututoa nje ya maji haya, hivyo tulikuwa tunaendelea kujisukuma kuogelea ili tusife”

Kitu pekee kinachoweza kukuzuia usifanikiwe ni ukuta ule unaouweka wa kusema hiki siwezi.

[  ] Amini kisha urudie mpango wako ulioshindwa haoo awali.

[  ] Jiamini na tengeneza ndoto yako kubwa ya maisha.

[  ] Jiamini, zidisha mara mbili lengo ulilolikamilisha sasa.

[  ] Jiamini unaweza kuikabili changamoto inayokuzuia sasa kama utatafuta kilichosahihi, kukifanya na kusubiri.

Kuna mengi ya kujifunza kuhusu uwezo mkubwa ulionao ndani yako na unavyoweza kuuamsha kisha kupiga hatua kubwa zaidi.

Ili uweze kuutambua uwezo huu na jinsi ya kuuamsha hakikisha umejipatia kitabu chako cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI. Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa nakala ngumu (hardcopy), nakala tete(Softcopy) na sauti(audiobook).

Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899 kupata nakala chache za ofa zilizobaki.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *