Jinasue Kwenye Mitego Hii Mitano Ili Kutengeneza Toleo Lako Bora Kuwahi Kutokea.
Nataka kuwa na maisha bora! Hili limekuwa ni tamanio la watu wengi ambalo halitimii.
Kwa sababu ya tamanio hili kutotimia kwa watu wengi, umefika wakati umejifariji kwa kuona kuwa maisha bora ni kwa ajili ya watu fulani wachache tu.
Kuwa na maisha bora na kuwa mtu yule uliyetarajiwa kuwa na kupata kile unachostahili ni haki yako ya msingi. Kila mtu anastahili kuwa na maisha bora lakini kabla ya kuwa na maisha hayo nje huna budi kuwa kwanza kuwa bora.
Ubora wa nje utategemea na ubora wa ndani. Kwa nini umeshindwa kuwa bora ndani yako kiasi cha kuathiri maisha yako ya nje?
Kuna mitego ambayo umenaswa nayo na hutakuwa bora mpaka umejinasua kwenye mitego hiyo kwanza. Ifahamu mitego mitano ambayo imekukamata na umeshindwa kuionyesha dunia toleo lako bora. Kisha anza kujinasua na mitego hiyo sasa.
- Kujilinganisha.
Unajilinganisha na nani? Kwani wewe unafanana na nani? Kwa kujilinganisha;
[ ] Umekosa furaha kwa kuona wewe huwezi.
[ ] Umejipunja kwani unejilinganisha na yeye aliyejipunja.
[ ] Umefanya matumizi ambayo hukupanga kuyafanya.
Wewe ni wa pekee sana, hulingani na mtu mwingine yoyote. Jitafute wewe halisi kisha jilinganishe na huyo. - Eneo huru(comfort zone).
Hakuna mambo makubwa unayoweza kufanya kama utaepuka maumivu na vitu vya kukutikisa ili kuwa na umakini muda wote. Usifanye ulivyovizoea tu hata kama havikupi matokeo unayoyataka.Jaribu vitu vipya na mbinu mpya. Chukua hatari kupata matokeo ya utofauti na makubwa zaidi. Anza kukifanya cha muhimu ulichokiogopa kwa siku nyingi. - Kukata tamaa.
Njia ya uhakika kabisa ya kushindwa ni kukata tamaa. Kama upo kwenye uelekeo sahihi kujisukuma na kukaa kwenye njia kwa muda mrefu, kutakufikisha mwisho. Endelea kulifanyia kazi lengo lako, vikwazo vitayeyuka na utaanza kupata matokeo. - Usumbufu.
Usumbufu gani unaruhusu maishani mwako? Je mitandao ya kijamiii inakula muda wako mzuri wa kufanya yale ya muhimu maishani mwako?
Je unaweka malengo, ungali unayatimiza fursa nyingine zinajitokea kukushawishi kuacha kila ulichokuwa unafanya hivyo umekuwa mtu wa kugusagusa tu mambo?
Zingatia kile unachokifanya huku ukizuia usumbufu wowote ule kukutoa kwenye reli.
- Kusubiri muda mzuri.
Leo ungekuwa mbali sana kwenye biashara yako kama ungeianza badala ya kusema unasubiri mambo yawe mazuri.
Ni kweli unahitaji kufanya maandalizi ya kufanya kitu, lakini kuna mambo mengi umeshindwa kuanza kwa kisingizio tu kuwa bado hujawa tayari.
Kuna mtu mmoja anaishi maisha ambayo unayatamani kuishi kwa sababu tu alipotamani maisha hayo, akachukua hatua. Maandalizi uliyonayo yanatosha, anza kazi sasa.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo wa kukuwezesha kupata toleo lako bora kwa kutambua upekee ulionao. Utakapotambua upekee ulionao utaamsha nguvu zako za kipekee zitakazokuwezesha kupiga hatua kubwa na kupata unachostahili.
Jipatie kitabu chako leo, utambue upekee wako haraka kama watu wengi walivyoshuhudia. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia kitabu hiki sasa.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz