Mtambue Mfalme Mkuu Wa Biashara Yako


Categories :

Kuna kitu kimoja ambacho kisipokuwepo kwenye biashara yako, biashara yako haitaweza kustahimili na hivyo kufa mapema tu.

Fedha ndiyo mfalme kwenye biashara yako, isipokuwepo, ni sawa na binadamu ambaye mzunguko wa damu mwilini mwake umesimama. Binadamu huyo hataweza kuishi, atakufa tu.

Hakikisha kila wakati baishara yako inatengeneza faida kwa fedha inayoonekana mkononi na siyo kwenye makaratasi. Unaposema biashara yangu inatengeneza faida, ione fedha hiyo mkononi mwako au ikiwa kwenye akaunti yako.

Kwa nini fedha ndiyo mfalme wa biashara yako?
1. Fedha ndiyo inanunua bidhaa au huduma ili wewe uuze.
2. Fedha ndiyo italipa mishahara wafanyakazi na hivyo kuendelea kufanya kazi kwa moyo.
3. Fedha ndiyo inayolipa kodi na bili mbalimbali.
4. Faida inayoonekana ndiyo inayokuhamasisha kufanya kazi.
5. Fedha ndiyo kitu pekee kinachozunguka kwenye biashara, isipokuwepo shughuli nyingi kwenye biashara yako hazitafanyika.

Ili mfalme huyu awepo kwenye biashara yako huku akilinda na kuikuza biashara yako, fanya yafuatayo;
1. Wateja wakulipe taslimu au ndani ya muda mfupi baada ya kuchukua bidhaa au kupata huduma.

2. Andaa mpango wa wateja kukulipa kidogo kudogo mpaka watakapomaliza kisha kuchukua bidhaa zako.

3. Ona uwezekano wa kununua bidhaa kwa mali kauli, lakini hakikisha unakuwa mwaminifu kulipa kwa wakati.

4. Kila siku kokotoa kujua faida kwenye biashara yako. Hii itakusaidia kujua kama mzunguko wa fedha ni chanya au hasi.

5. Jiandae kukabiliana na matumizi makubwa kama vile kulipa kodi ya pango, mapato nk. Anza kukusanya fedha hii taratibu ili isitoe damu yote kwenye biashara yako.

Ifanyie tathmini biashara yako, je unaionaje hali ya mfalme huyu wa biashara yako?

Kama fedha inayotoka ni nyingi kuliko inayoingia, basi ziba mianya hiyo kwanza. Kisha anza kutumia mbinu hizo hapo kuhakikisha biashara yako inavuta fedha na kutengeneza fedha kila wakati.

Ili kujifunza zaidi kuhusu mzunguko wa fedha kwenye biashara yako na namna ya kukokotoa faida na kukuza biashara yako,  hakikisha unajipatia kitabu chako cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA.

Maarifa yaliyopo kwenye kitabu hiki ni rahisi kuyaelewa na kuyatumia hivyo utaanza kupata matokeo chanya mapema. Wasiliana kupitia namba 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *