Kumbukumbu Tano Zinazokimbiza Chumaulete Kwenye Biashara Yako Kisha Kuanza Kuiona Faida Kwenye Biashara Yako.


Categories :

Je umefanya biashara yako kwa muda mrefu lakini huoni ikikua kiasi cha kuamini kuna chumaulete kwenye biashara yako?

Je unahisi unafanya mauzo makubwa lakini ukitoa fedha kwenye biashara yako, biashara yako inatetereka?

Hapo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na chumaulete kwenye biashara yako. Na usipomthibiti mapema biashara yako itakufa kama biashara nyingine nyingi zilivyokufa.

Habari njema ni kuwa una uwezo wa kumuona wazi chumaulete wa biashara yako kama utafanikiwa kuweka kumbukumbu hizi tano kwenye biashara yako;

1. Manunuzi Yote.
Manunuzi ni kitu kinachotoa fedha kwenye biashara yako. Rekodi kila manunuzi ya bidhaa au huduma unayofanya. Fanya hivyo kila unapofanya manunuzi, usiseme nitafanya baadaye,  utasahau.

2. Mauzo.
Ili uweze kujua faida ghafi na baadaye halisi ya biashara yako, hakikisha unarekodi kila mauzo unayofanya.  Rekodi hii iainishe bei ya kununulia, bei ya kuuzia na faida ghafi kwa kila bidhaa au huduma unayotoa.

3. Matumizi.
Rekodi hii huonyesha fedha vinavyotoka kwenye kikapu cha biashara yako bila kurudi. Ni rahisi sana kumsingizia jirani yako kuwa ni chumaulete kama huweki kumbukumbu za matumizi.  Rekodi matumizi yoyote yale yanayotoa fedha kwenye biashara yako kama; kodi ya pango, usafi, bili za maji na umeme, mishahara….. hata fedha unayojikopesha bila kurudisha! Usujali udogo wake..

4. Madeni.
Andika orodha ya watu wote unaowadai na siku walizoahidi kulipa. Usiporekodi kisha  kufuatilia madeni hayo, unatengeneza chumaulete kwenye biashara yako. Lakini pia kumbuka kurekodi madeni yote unayodaiwa.

5. Faida.
Ili kutambua kuwa biashara yako itaendelea kuwepo na kukua au itakufa, huna budi kuwa na kumbukumbu hii kila siku, wiki na mwezi. Kuna aina mbili za faida; ghafi na halisi.
Faida ghafi = Mauzo – Manunuzi.
Faida halisi = Faidha ghafi – Matumizi.

Kumbuka utaweza kukokotoa faida kama utakuwa umeweka kumbukumbu za manunuzi, mauzo na matumizi vizuri.

Pata picha unaifahamu faida ambayo biashara yako inapata kisha ukaweka mikakati mikubwa zaidi kuikuza, utajisikiaje?

Naamini utajisikia vizuri.  Anza leo kuweka kila kumbukumbu inayohitajika kuwekwa kwenye biashara yako. Anza hata kurekodi kwenye kitabu cha biashara yako ungali unatafuta mfumo wa kielekteoniki.

Hata hivyo kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA kimeelezea kiundani zaidi namna ya kuweka kumbukumbu vizuri kwenye biashara yako.

Kina mfano wa majedwali unayoweza kuchora kwenye daftari lako kisha kurekodi kumbukumbu hizo muhimu kiurahisi. Hii itakuwa chachu kubwa sana kwenye ukuuaji wa biashara yako.

Habari njema ni kuwa kuna nakala chache za ofa zimebaki unazoweza kuwahi leo. Kuiwahi ofa hii wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *