Hiki Ndicho Kimekuwa Kinakuzuia Usipate Unachostahili. Ifahamu Njia Ya Uhakika Ya Kukusaidia Kutoka Hapo…
Kipato unchokipata sicho unachostahili, ndiyo maana huridhiki nacho.
Kasi ya mafanikio siyo unayostahili, ndiyo maana umeachwa mbali sana na mahitaji ya fedha.
Hali ya biashara yako siyo unayostahili, ndiyo maana ni kama ipo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi(ICU).
Malengo yako uliyonayo siyo unayostahili ndiyo maana huamushi nguvu kubwa ndani yako na hivyo umepata matokeo kidogo sana kuliko unayostahili.
Hamasa uliyonayo ni ya muda tu ndiyo maana una siku chache unazokuwa na shauku ya kufanya na kupata makubwa maishani mwako. Hii imekufanya kuwa mtu wa kawaida tu.
Ndugu Bruce Lee alisema ”You will never get any more out of life than you expect” ikiwa na tafsiri kuwa “Hutapata zaidi kwenye maisha zaidi ya kile unachokitaraji”
Akili yako imeweka viwango vya nini unastahili kwenye kila eneo la maisha yako. Hiki unachokipata ni kile ambacho akili yako inakiamini.
Hiki unachopambania na kukipata ni kile ambacho akili yako inakiamini.
Hata kama huridhiki utaendelea na hali hiyo maishani mpaka pale akili yako itakapoona na kuamini kuliko sasa.
Usiendelee kulalamika kuhusu hali yako. Usiendelee kujiona wewe huna bahati.
Usiridhike na kushindwa ukiamini wewe ni fungu la kukosa.
La hasha! Kuna jambo moja muhimu la kufanya kisha maamuzi, vitendo na matokeo vitabadilika mara moja.
Jambo hilo ni kubadili matarajio yako. Bruce Lee amekukumbusha kuwa hutapata zaidi kile unachokitarajia.
Ndani yako kuna nguvu kubwa ya kufanya zaidi ya sasa, lakini kuiamsha nguvu hii unahitaji kubadili mtazamo wako kwanza kiasi cha kugundua ni kwa kiasi gani umejipunja kwa muda mrefu.
Uliumbwa na nguvu kubwa ndani yako na umetumia chini ya 10%. Hivyo zaidi ya 90% ya nguvu zako zipo tu ndani yako zimelala.
Utajisikiaje kama leo utatambua njia za kuamsha nguvu zako hata kwa 1% na kupata matokeo makubwa ambayo hujawahi kuyapata? Naamini utajisikia vizuri.
Hata hivyo kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ndiyo mwongozo pekee utakaokuongoza kuamsha uwezo wako na kuanza kufanya mambo makubwa uliyoshindwa kwa muda mrefu.
Jipatie nakala ya kitabu hiki kwa bei ya ofa. Nakala ngumu(hardcopy) sh 15,000/, nakala tete(softcopy) sh 10,000/ na nakala ya kusikiliza (AUDIOBOOK) sh 10,000/. Ungependa ujipatie nakala gani leo? Wasiliana kupitia 0752 206 899 kuwahi ofa yako.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz