Hivi Ndivyo Unavyochimba Kaburi La Kuzika Ndoto Zako. Okoa Uhai Wa Ndoto Zako Sasa…
Kwa nini hakuna dalili yoyote ya kutimiza ndoto za maisha yako ambazo zingekupa thamani kubwa ya uwepo hapa duniani?
Kwa nini umekuwa ukiweka malengo yaleyale miaka nenda miaka rudi bila kuyatimiza?
Kwa nini kila ukipanga kufanya kitu umekuwa ukiahirisha kabla aua muda mfupi tu baada ya kuanza kufanya?
Kwa nini unapokuwa na mipango mizuri ya kukupa matokeo makubwa umekuwa ukiogopa kuchukua hatua kwa sababu ni kitu ambacho hujazoea kufanya?
Ndugu! Huku ni kuzika ndoto zako na anayechimba kaburi la kutumbukiza ndoto zako ni wewe mwenyewe.
Unaweza ukajiuliza ni wapi huko nachimba kaburi hilo? Hili ndilo jibu;
Kuendelea kung’ang’ania kubaki kwenye eneo huru (comfort zone) ni kuchimba kaburi la ndoto zako.
Kung’ang’ana kwenye comfort zone ni;
[ ] Kutotaka kujisumbua.
[ ] Kutotaka kujisikuma.
[ ] Kutotaka kuumiza kichwa.
[ ] Kutotaka kutoka kwenye mazoea.
[ ] Kutotaka kujaribu.
[ ] Kutotaka kuaibika.
[ ] Kutotaka kukataliwa.
[ ] Kutotaka kushindwa.
[ ] Kukimbia hofu.
[ ] Kufanya ulicho na uhakika.
Naomba nikuambie ukweli kuwa hakuna maajabu yoyote utakayoyapata maishani mwako kwa kuendelea kubaki kwenye comfort zone zaidi ya kuzika ukubwa uliotegemewa kuuonyesha hapa duniani.
Mwaka 2023 umezika ndoto zako vya kutosha. Anza sasa kufufua ndoto zako ili mwaka 2024 unapofika ukute ndoto zako zikiwa hai kisha uendelee kuzikuza.
- Fanya kile unachoogopa kukifanya lakini chenye manufaa..
- Fanya kile ulichokiashirisha mara nyingi.
- Fanya kile kinachokupa maumivu.
- Fanya kile kitakachokuhitaji ufikiri zaidi.
- Fanya kile kitakachokupa matokeo bora zaidi ya jana.
- Fanya kile kitakachokuonyesha upekee wako.
- Fanya kile kitakachokupa jina(Brand).
- Fanya kile ambacho hata ukifa dunia itaendelea kukuishi.
- Fanya kile kitakachokutoa jasho hata kama upo kwenye kiyoyozi.
- Fanya kile ambacho kitahitaji fikra zako, uzingativu wako na hisia zako kuwepo pale.
NB: Fanya kile ambacho hata wewe utashangaa ukubwa wa matokeo yake.
By the way kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo utakaokusaidia kuamsha nguvu ya kujisukuma ili kutimiza malengo yako.
Mwongozo huu unakusaidia kuacha kutoa sababu kwenye kile ulichopanga kufanya bali kuanza kutoa matokeo.
Habari njema ni kuwa leo utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz