Kitu Pekee Kinachoweza Kukusaidia Kuchukua Hatua Ngumu Za Kukupa Mafanikio Mkubwa…


Categories :

Hakuna mafanikio makubwa bila kupitia hatua ngumu. Changamoto kubwa zinaposimama mbele yako ndipo wewe huamua kuwa ukipate kile unachokitaka au la!

Kama kuna watu hawajapata vile walivyosema wanavitaka na sasa huoni jitihada zozote basi tambua kuwa changamoto zimewawashinda.

Kadhalika kama kuna kitu ulipanga kukipata lakini hujapata na umeacha kuchukua hatua basi tambua kuwa changamoto hiyo imeibuka kuwa mshindi juu yako.

Hakuna miujiza yoyote ya kupata matokeo kama hutafanya bidii kuwa juu ya vikwazo vinavyokuzuia.

Baada ya magumu au changamoto kusimama mbele ya mipango ya kutimiza malengo yako, ndipo sababu za kutokuchukua hatua hujitokeza sababu hizo ni kama:
[  ] Kuna njia ya mkato naweza kuipata.
[  ] Nitajaribu kesho, kesho inaweza kuwa rahisi.
[  ] Sina haja ya kujitesa.
[  ] Mbona watu wengi tu wameshindwa!

Kuna kitu kimoja muhimu cha kufanya ili uwe mtu wa kuchukua hatua. Kitu hicho ni kutafuta KWA NINI KUBWA ya kufanya kitu hicho.

KWA NINI KUBWA ni sababu inayokufanya uchukue hatua. Sababu ya kuchukua  hatua lazima iwe kubwa kushinda sababu inayokushwawishi uache.

Kwenye kila hatua muhimu ya kuchukua tafuta na weka wazi kabisa KWA NINI KUBWA ya kufanya kitu hicho.

[  ] Kwa nini uamke mapema….je ni kwa sababu utapata muda wa kuipangilia siku yako vizuri na kuwa na uzalishaji mkubwa?

[  ] Kwa nini usiahirishe kazi mwili unapojisikia uvivu?….je ni kwa sababu unahitaji matokeo ya kazi hiyo yakutoe kwenye hali mbaya ya kiuchumi uliyonayo.

[  ] Kwa nini ujisukume kufanya kile unachokihofia?….Je ni kwa sababu umechoka na matokeo yaleyale ya kawaida kila siku?

[  ] Kwa nini ujibane kutumia kipato chote? ..je ni kwa sababu kuweka akiba ndiyo njia pekee ya kufikia uhuru wa kifedha?

[  ] Kwa nini ujisukume kuanzisha biashara licha ya hofu ya kupoteza mtaji? … Je ni kwa sababu biashara ndiyo njia pekee ya kukuza kipato chako kwa haraka?

Kwenye kila lengo ulilopanga kufanyia kazi mwaka huu weka bayana KWA NINI KUBWA na pale sababu za kutokuchukua hatua zinapokujia, jikumbushe kwa nini kubwa ya kufanya kitu hicho. Ndipo utakapokuwa na mwaka wa mafanikio makubwa.

Hata hivyo kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo muhimu wa kukufanya kuwa mtu wa kutoa MATOKEO na siyo SABABU.

Habari njema ni kuwa kitabu hiki bado kinapatikana kwa bei ya ofa ya mwaka mpya. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kuwahi nakala chache za ofa zilizobaki.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *