Jinsi Unavyokuwa Chuma Ulete Wa Biashara(Fedha) Yako. Fanya Hivi Kulinda Fedha Zako….


Categories :

Je kila ukipata fedha baada ya muda mfupi tu huzioni  fedha hizo na unahisi kuna chuma ulete anachukua fedha zako kiuchawi?

Je una biashara na unafanya mauzo lakini fedha huzioni kiasi cha biashara kubaki palepale au ndiyo kuanza kufa?

Kama haya yanatokea maishani mwako, naamini utakuwa tayari umeanza kumatafuta au kuhisi chuma ulete wa biashara yako.

Lakini kama hufanyi yafuatayo, nasikitika kukuambia kuwa chuma ulete namba moja wa fedha zako utakuwa wewe mwenyewe ;

  1. Kama hujui kipato au mauzo unayofanya basi wewe ndiyo chuma ulete mwenyewe.
  2. Kama unafanya mauzo bila kuandika basi unamtengeneza chuma ulete kwenye mauzo yako.
  3. Kama unafanya manunuzi bila kuweka kumbukumbu basi wewe ndiyo chumaulete.
  4. Kama unafanya matumizi bila bajeti basi wewe ndiyo chuma ulete.
  5. Kama una bajeti lakini hauifuati basi wewe ndiyo chuma ulete.
  6. Kama hujui biashara yako inatengeneza faida au la basi tambua ndiyo unamtengeneza chuma ulete.

Kama hutaki kuwa chuma ulete basi fanya yafuatayo;

  1. Rekodi kila kipato unachoingiza au kila mauzo unayofanya.
  2. Weka bajeti ya matumizi ya maisha au biashara yako.
  3. Jenga nidhamu kali ya kuishi kwenye bajeti yako.
  4. Usitumie zaidi ya kipato chako.
  5. Jifanyie tathmini ya matumizi mara kwa mara.
  6. Jua namna ya kukokotoa faida au hasara ya biashara yako.
  7. Andaa mgawanyo wa fedha zako kabla hujazipata.

Hata hivyo kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA kimeelezea kiundani jinsi unavyoweza kuthibiti chumaulete kwenye biashara yako kisha kuweza kuiona faida au hasara inayotengenezwa na biashara yako.

Kupitia maarifa haya utaweza kukuza biashara yako kisha kukupa kipato kitakachokufikisha kwenye uhuru wa kifedha.

Kuna nakala chache za ofa ya mwaka mpya zimebaki. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa kwa bei ya ofa.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *