Kama Unataka Utoke Mwaka 2024 Hakikisha Unakifanya Hiki.


Categories :

“Kifaranga hufanikiwa kukua kisha kutoka  nje ya ganda la yai kwa sababu ya kubaki hai”

Kama kifaranga kitakufa kingali kipo ndani ya yai, basi hakitaweza kutoka nje.

Lengo lako kuu la mwaka 2024 litakutana na changamoto  nyingi sana. Utakutana na vikwazo vingi vitakavyotaka kuua matarajio uliyonayo.

Kuna namna moja tu ya kufanikiwa kutoka na kuwa mshindi mwaka 2024, nayo ni kubakia hai hata pale changamoto zitakaposimama mbele ya malengo yako na kukutaka kuua matarajio yako.

Usikubali changamoto yoyote ile iue ndoto yako ya mwaka 2024.

  1. Fursa nyingine ikijitokeza usikubali kuacha lengo lako ukahamia lengo jingine. Baki hai.
  2. Utakapopanga kuchukua hatua kwa ajili ya kutimiza lengo lako, usiahirishe. Baki hai
  3. Matokeo ya mipango yako yatakapochelewa vumilia, endelea kuchukua hatua. Baki hai.
  4. Utakapochukua hatua na kushindwa, usiache; jifunze na rudi ukiwa bora. Baki hai.
  5. Watu watakapokuambia huwezi kutimiza lengo lako,  usiwasikilize; jiambie nina nguvu kubwa ndani yangu bado imelala tu, nitaiamsha na kufanya makubwa. Baki hai.
  6. Utakapopata matokeo kidogo usiridhike bali shukuru kisha pata nguvu ya kuendelea ili kutimiza lengo zima. Baki hai.

Visababishi  hivi na vingine vinavyofanana na hivi vya kushindwa kupata matokeo ya malengo yako vitakapojitokeza, usife endelea kubaki hai.

Utatoka na kufanikiwa mwaka 2024 kwa kuendelea kubaki hai.  Kamwe  usikubali kufa kwa kukubali kushindwa.

Utafanikiwa kutoka kama utaendelea kujisukuma hata pale mambo yanapokuwa magumu au utakapokuwa hujisikii kabisa kuchukua hatua.

Hata hivyo kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo kwako kukusaidia kuamsha nguvu ya kujisukuma ili kuchukua hatua hata pale vikwazo vitakapoibuka.

Ukifanikiwa kuamsha nguvu hii, hutatoa SABABU ya kwa nini usichukue hatua na kupata matokeo bali utatoa MATOKEO kisha kutimiza malengo yako.

Jipatie nakala yako leo upate uhakika wa kutoka mwaka 2024. Kuna nakala chache sana za ofa ya mwaka mpya utazipata leo.

Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *