Kama Hujafanya Kitu Hiki Kwenye Malengo Yako, Basi Tambua Kuwa Huna Malengo. Lakini Unaweza Kukifanya Sasa…..
Hongera kwa kuwa na shauku ya kufanya makubwa mwaka 2024.
Hongera kwa kutambua kuwa mwakajana hukufanya vizuri na hivyo una nafasi ha kufanya vizuri mwaka huu.
Hongera kwa malengo uliyonayo mwaka 2024.
Je umeyaandika malengo yako?
Moja ya kigezo cha wewe kuweza kulitimiza lengo lako, ni lengo hilo kuwa wazi kabisa.
“Lengo lisiloandikwa ni tamanio tu”
Akili yako lazima ione picha kamili ya nini hasa unakitaka na kwa namna gani utakipata.
Njia pekee ya lengo kuwa wazi kabisa kisha akili na asili vikawa tayari kukuwezesha kutimiza ni kwa kuyaandika malengo yako.
Kwa kutoyaandika malengo, watu wengi husahau kabisa walipanga kufanya nini baada ya miezi miwili tu tangu waweke malengo yao.
Faida za kuandika malengo yako ni;
[ ] Akili yako inalielewa lengo lako na kuwa rahisi kuchukua hatua.
[ ] Unakuwa na hamasa ya kudumu
[ ] Inakuwa rahisi kuyakumbuka malengo yako.
[ ] Ni rahisi kujifanyia tathmini.
[ ] Malengo yako yatakaa kichwani na itakuwa rahisi kutembea nayo.
Kuna nafasi kubwa kwako ya kufanikiwa kama utaweka malengo kuliko usipoweka. Lakini nafasi hiyo inaongezeka pale unapoyaandika malengo yako.
Unasema una malengo ya mwak 2024, yako wapi?
Chukua hatua.
Andaa kitabu kwa ajili ya maisha yako kisha andika malengo yako ya mwaka 2024.
Usiandike mara maoja bali kila siku mpaka akili yako iyakariri.
Nakutakia kila la kheri katika kuyaandika na kuyatimiza malengo yako.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz