Ni Jambo Lenye Maumivu Lakini Huna Budi Kulifanya Ili Upate Fedha Zaidi…..
Moja ya nguvu za mvutano alizonazo mwanadamu na vitu, ni kati ya yeye na fedha zake.
Hivyo moja ya kitu ambacho mtu hapendi kukitoa kirahisi ni fedha zake.
Hii imeenda mbali zaidi; mtu hataki hata kutoa fedha ili imuzalishie zaidi.
Kwa sababu ya kung’ang’ania kukaa na fedha bila kuzitoa, ndipo nguvu kubwa ya mtumizi huzifuata fedha hizo na mtu kuishia kutumia fedha zote bila ya kutoa na kuweka sehemu ambazo zingezalisha zaidi.
Ili uweze kufikia uhuru wa kifedha, huna budi kuzitoa fedha na kuweka maeneo yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ili uweze kupata fedha zaidi.
Kama kipato chako kimekuwa hakiongezeki sababu mojawapo inaweza kuwa ni kutokuwa tayari kutoa fedha ili zikuzalishie zaidi.
Hivi ndivyo unavyoweza kutoa fedha mikononi mwako ili zikuzalishie zaidi;
[ ] Lipa ili ujifunze. Maarifa ni gharama, lakini ukijifunza utatoa thamani kubwa zaidi na utalipwa zaidi.
[ ] Wekeza kwenye hisa, vipande, hati fungani ili thamani iongezeke. Mwanzoni inaweza kuonekana kama umepoteza fedha, lakini kadri muda unavyokwenda utaiona faida yake.
[ ] Weka fedha kwenye biashara , unaweza kupata hasara mwanzoni lakini ndiyo njia ya kujenga biashara ya kukupa uhuru wa kipato.
[ ] Biashara ni umaarufu wa jina(Brand); toa fedha kutengeneza jina kwa uaminifu mkubwa kisha kuza thamani na mauzo yako.
[ ] Tumia fedha kufanya matangazo; watu wakiifahamu biashara yako, watanunua zaidi na utafaidika zaidi.
Ni eneo gani utaanza kutoa fedha zako kwanza ili uzalishe kipato chako zaidi?
Anza Leo Anza Sasa Anza na Ulichonacho.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz