Tabia Tano Unazoweza Kuanza Kuziishi Leo  Kisha Zikakusaidia Kutimiza Malengo Yako mwaka 2024.


Categories :

Kama kuna kitu kinachoweza kukuhakikishia kutimiza malengo yako basi ni tabia. Tabia ni vitu unavyoweza kuvifanya kila siku au kila wakati. Anza kujenga tabia hizi tano zitakazokuwezesha kuana kutimiza malengo yako mwaka 2024 na baada ya hapo.

1. Amka Mapema.

Kuna methali inasema ‘’The early bird cathches the worm’’ ikiwa nat afsiri kuwa ndege anayekuwa wa kwanza ndiye anayekamata mnyoo. Kwa kuhawahi kuamka kuna vitu unavyovipata kuliko anayechelewa.

Kuamka saa 11 asubuhi au kabla ya hapo kunkupa faida ya

[  ] Kufanya mazoezi ya mwili
[  ] Kuipangilia siku yako
[  ] Kusoma vitabu

2. Andika kabla hujalala.

Mina Murray alisema kuandika ” Journaling is like whispering to one’s self and listening at the same time” ikiwa na tafsiri kuwa Kuandika habari ni kama kujinong’oneza na kusikiliza kwa wakati mmoja”. Kabla ya kulala

[  ] Andika malengo yako ya kesho
[  ] Shukuru kwa siku inayoenda kuisha
[  ] Andika mambo uliyojifunza

Kwa kufanya hivyo utakuw ana usingizi mzuri na kukusaidia kuamka asubuhi ukiwa na nguvu.

3.Tumia dakikia 30 kila siku kujifunza ujuzi kwenye mtandao.

Malcolm X  alisema “Education is the passport to the future, for tomorrow belongs to those who prepare for it today.” ikiwa na tafsiri kuwa “Elimu ni pasipoti ya siku zijazo, kwa maana kesho ni ya wale wanaoitayarisha leo.”

Ujuzi ndiyo utakaokupa fedha kisha utajiri. Tenga dakika 30 kila siku na jifunze yafuatayo;
[  ] Masoko mitandaoni.
[  ] Uandishi.
[  ]  Ushawishi.
[  ] Kufanya maamuzi sahihi

4. Tembea dakika 30 kwenye mazingira ya asili.

John Muir alisema ‘In every walk with Nature one receives far more than he seeks.’ ikiwa na tafsiri kuwa
‘Katika kila kutembea kwenye mazingira ya asili mtu hupokea zaidi ya anavyotafuta.’ Kuna faida kubwa sana ya kutenga muda kisha kutembea kwenye mazingira tulivu ya asili. Hii ni fursa ya kusikia ambavyo hujawahi kuvisikia au kuvihisi.

Kwa kutembea huko;

[  ] Utaepuka ‘stress’
[  ] Utaongeza furaha
[  ] Utajisikia vizuri(mood)

5. Soma kurasa 10 kila siku.
Joseph Addison alisema “Reading is to the mind what exercise is to the body.” ikiwa na tafsiri kuwa “Kusoma ni kwa ajili ya akili kama  jinsi mazoezi yalivyo kwa ajili ya mwili.”

Kama unataka akili yako ifanye kazi kwenye viwango vya juu na kukupa mafanikio, hun budi kuifanyisha mazoezi kwa kusom kila siku.

kusoma kutakusaidia;

[  ] Kuongeza uzingativu wako hivyo kuwa na uzalishaji mkubwa.
[  ] Kuongeza maarifa hivyo kukuwezesha kufanya vitu kwa ushaihi.
[  ] Kuongeza kujiamini kwa sababu unakuwa na taarifa sahihi.

Rafiki yangu! Anza kuishi leo tabia hizi tano bila kuacha hata siku moja, hakika utaanza kuona mabadiliko makubwa sana maishani mwako.

Hata hivyo kuna orodha ya vitabu unavyoweza kuanza kusoma leo.

  1. AMSHA UWEZO WAKO HALISI
  2. DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO
  3. UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA
  4. JENGA NIDHAMU KALI.

Kitabu gani ungependa kuanza kukisoma leo. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia kitabu chako leo.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *