Ni Kama Kitu Kidogo Vile Lakini Nidiyo Chanzo Cha Utajiri Maishani Mwako.
Ni kitu ambacho hujazoea lakini kifanye.
Ni tabia ngumu lakini wewe ijenge.
Ulitakiwa uanze miaka mingi nyuma lakini muda mwingine ni LEO.
Matajiri wote unaowaona ndicho wanachofanya.
Huhitaji uwe na fedha nyingi unaweza kuanza na kile ulichonacho.
Si uwingi wa unachopata bali ni tabia.
Kama sijawahi kukuambia basi leo siri nakupa.
Kama nimewahi kukuambia basi leo nakukumbusha siri hiyo.
Kitu hicho kidogo ni KUJILIPA WEWE KWANZA kwenye kila kipato unachopata.
Ukipata fedha usitumie yote. Jilipe kwanza.
Iwe ndogo au kubwa, jilipe kwanza.
Ukijilipa weka sehemu ambayo haitapungua bali itaongezeka.
Kadri unavyoweka itazidi kukua na kukufanyia kazi ya kukuzalia fedha nyingine bila ya wewe kushika jembe.
Kama kuna habari njema kubwa umewahi kusikia hii ni mojawapo.
Kama kuna kitu cha kuanza kufanyia kazi haraka ili kujenga uhuru wa kifedha basi ni hiki.
Anza leo kutoa 10% ya kila kipato na kuweka sehemu itakazalisha zaidi. Kama 10% ni kubwa basi 5%, kama tano bado kubwa basi 2% au 1%. Kujilipa si kipato bali ni tabia. Anza leo.
Miaka 20 utajuta kwa kutofuata ushauri huu au utajipongeza kwa kuwa ni tajiri kwa kufuata ushauri huu.
Anza Leo Anza Sasa Anza Na Ulichonacho.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
.