Kama Unakata Tamaa Kwenye Mambo Yako, Basi Tambua Kuwa Hiki KITU Hakipo Sawa.


Categories :

Je umeshindwa kuamka mapema kwa kisingizio kuwa usingizi wa asubuhi ni mtamu na kuna akili inakuambia kwa nini ujitese?

Je umeweka malengo madogo ukiwa na wasiwasi kuwa makubwa utayatimizaje?

Je umeanza kutimiza malengo lakini ukakata tamaa kwa sababu umekutana na magumu?

Je hujaanza kuishi ndoto yako kwa sababu unahofia watu watakuchukuliaje?

Je kuna mteja mwenye uwezo wa kununua kwenye biashara yako lakini hujamwendea kwa sababu unaogopa atakataa?

Je unaogopa kuanzisha biashara kwa sababu unahisi utapata hasara?

Je hujaanza kuweka 10% ya kila kipato chako kwa kisingizio kuwa kipato chako ni kidogo?

Rafiki! Kama majibu ya maswali hapo juu ni ndiyo basi rejea nukuu ya Jim Rohn hapa chini;

Jim Rohn alisema “If the WHY is powerful,  the HOW is easy.” ikiwa na tafsiri kuwa kama KWA NINI in nguvu basi KWA NJIA GANI inakuwa rahisi.

Kama kuna kitu hukifanyi, si kwa sababu huna uwezo au haiwezekani,  bali ni kwa sababu KWA NINI ya kufanya kitu hicho haijawa kubwa kiasi cha kurahisisha kupata njia.

Kwenye kila kitu ambacho umekuwa ukisita kuanza au ulianza kisha kukata tamaa, hujapata SABABU KUBWA ya kwa nini ukifanye!

Kwa mfano KWA NINI ya kuweka akiba ni inaweza kuwa ni kuepuka shida za kifedha unazoweza kupata pale utakapokuwa huna nguvu za kufanya kazi kisha kuingiza fedha kila siku.

Chukua hatua LEO.

  1. Ainisha malengo uliyokuwa unafanyia kazi kisha ukakata tamaa kwa sababu ya kuona haiwezekani.

AU
Malengo ambayo umekuwa ukiyaogopa kuyaanza kwa sababu ya kuona huna uwezo nayo.

  1. Kwenye kila lengo ainisha KWA NINI KUBWA ya kufanya kile unachotaka. Ni kitu gani kizuri sana utakipata au maumivu gani makubwa utayaepuka?
  2. Jiulize  ni kwa namna gani utapata hicho unachokipata.

Karibu nishirikishe lengo moja tu kubwa ambalo unalo na kwa nini kubwa ya kuliendea lengo hilo na kwa njia gani.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *