Jitahidi Upate Akili Hii Ya Fedha Itakayoifanya Fedha Yako Ikue Kwa Maajabu Makubwa.
Kama ulikuwa unafikiri kuna maajabu saba tu ya dunia, basi utakuwa unajidanganya mwenyewe.
Kuna ajabu jingine kati ya maajabu yale saba ya dunia unayoyafahamu. Ajabu hilo linahusu fedha.
Habari njema ni kuwa na wewe una uwezo wa kulitengeneza ajabu hilo. Hutafaidika kwa kujenga ajabu hilo tu bali utapata faida ya moja kwa moja ya fedha yako kukua kimaajabu sana.
Albert Einstein alisema “Compound interest is the eighth wonder of the world. He who understands it, earns it; he who doesn’t, pays it.” I kiwa na tafsiri kuwa riba mkusanyiko ni ajabu la nane la dunia. Yule anayeielewa anafaidika nayo, yule asiyeielewa anajutia.
Riba mkusanyiko ina maajabu makubwa sana kiasi cha kumshawishi mwanasayansi nguli, Albert Einstein kuona hilo ni ajabu la nane la dunia.
Unaweza ukawa unajiuliza Riba Mkusanyiko(Compound interest) ni kitu gani? Usiwe na wasiwasi, leo utaifahamu hii kisha kuamua kuanza kuitumia ili uanze kuifaidi.
Riba mkusanyiko ni aina ya riba ambayo na yenyewe baada ya kupatikana huungana na mtaji wako kuzalisha riba nyingine kubwa zaidi kuliko ile ya kwanza.
Kwa mfano kama umewekeza sh. 1,000,000/ kwenye taasisi inayotoa riba ya 10% kwa mwaka na yenye sifa ya riba mkusanyiko basi fahamu kuwa mwishoni mwa mwaka utakuwa umepata riba ya sh. 100,000/.
Sasa kwa sifa ya riba mkusanyiko, mwaka unofuata hutakuwa na mtaji wa sh. 1,000,000/ tu bali utakuwa 1,100,000/ kwani ile riba yako itaingana na mtaji wako kuzalisha riba nyingine. Ambapo mwaka wa pili riba yake haitakuwa 100,000/ bali 110,000/. Na riba hii ya sh 110,000/ itaungana na mtaji wako wa sh 1,100,000/ na kufanya kuwa sh. 1,210,000/ kama mtaji unawekeza mwaka tatu.
Mchezo huu utaendelea kufanyika kadri miaka inavyoenda na kufanya fedha yako ikue kwa kasi ya ajabu.
Kuufahamu huu mchezo wa riba mkusanyiko ni akili muhimu sana ya kifedha katika kujenga uhuru wako wa kifedha.
Kwa kutambua umuhimu wa jambo hili, AMSHAUWEZO Consultants imekuandalia semina kuhusu SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA ambapo pamoja na masomo mengi yenye thamani kubwa kuhusu fedha, utajifunza pia ajabu hili la nane la dunia.
Semina hii itafanyika kwa siku 10 kwa njia ya kundi maalumu la wasap kuanzia tar 18.03.2024 mpaka 27.03.2024.
Hiki ni kitu unachohitaji sana maishani mwako. Fursa na wakati vimefika, ni sasa. Ada ya semina hii ni sh. 10,000/ yaani sh 1,000/ tu kwa siku. Hii ni bahati kwako. Fanya malipo yako kwa mpesa: 0752 206 899(Alfred Mwanyika).
Ili kujihakikishia nafasi chache zilizopo jiunge sasa kwa kubonyeza kiunganishi hiki https://chat.whatsapp.com/Lmel6ehEr30K5a1S1BCEYu
Usipange kukosa. Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na;
Mwl. Alfred Mwanyika,
CEO: AMSHAUWEZO Consultants,
Simu: 0752 206 899: Email: alfredgeofrey@gamail.com
www.amshauwezo.co.tz
Karibu sana.