Kuwa Na Vitu Hivi Viwili, Fedha Zitakufuata Ulipo.


Categories :

Je Unataka Fedha Zitiririke Kuja Kwako?

Kama kuna kitu ambacho mtu anatamani akipate kwa wingi, basi ni fedha.

Lakini kama kuna kitu ambacho watu wanakipata kwa uchache basi ni fedha.

Fedha zimejificha wapi?

Kwenye makala iliyopita tuliona kuwa hakuna fedha iliyoitoroka dunia na kwenda sayari nyingine.  Fedha zote zipo hapahapa duniani.

Lakini je zimejificha wapi?

Fedha zimejificha kwenye Bidhaa au Huduma.

Tafakari kwa muda! Ni wapi fedha zako za miezi mitatu(Januari, Februari na Machi) ya mwaka 2024 umezitumia.

Naweza kukisia kuwa 90% mpaka 100% ya fedha zako zote umetumia kwenye kununua bidhaa au kulipia huduma.

Umenunua nguo, chakula, malazi, simu, vocha, samani, chombo cha usafiri,……Lakini pia umelipa ada za shule, kodi ya nyumba, umeme(LUKU), king’amuzi,…..

Kumbe fedha zinatoka kwa watu na kufuata bidhaa na huduma ziliko. Kama unatafuta fedha ziliko, basi tambua kuwa zimejificha kwenye bidhaa au huduma.

Hivyo kama unataka zije kwako, basi hakikisha una bidhaa au huduma. Na kama zinakuja kidogo basi ongeza uwingi au ubora wa bidhaa na huduma unazozitoa.

Chukua Hatua Leo.

  1. Angalia ni bidha au huduma gani inayokosekana maeneo unayoishi au mengine kisha leta bidhaa au huduma hiyo. Watangazie watu kuwa sasa bidhaa na huduma walizokuwa wanakosa sasa zinapatikana. Hapo ndipo fedha zitakapoanza kutiririka kwako.
  2. AU Angalia bidhaa au huduma unazozitoa sasa. Kama huridhiki na fedha zinazokuja kwako, basi ongeza ubora, uwingi na kufanya masoko zaidi. Hapa ndipo fedha zitakapoongezeka kutiririka kwako.

Chukua hatua hizo mbili muhimu kuongeza kipato chako.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *