Je Unataka Matokeo Ya Utofauti Maishani Mwako? Basi Fanya Hivi….
Kuna mazingira uliyoyazoea ndiyo yaliyoyaweka jela maisha yako.
Miaka mingi inapita lakini bado upo palepale.
Umetafuta mchawi wa maisha yako, ukampata jirani. Lakini maisha yako yapo palepale.
Hali ya kifedha, mahusiano, biashara, uwekezaji…..imebaki palepale.
Unataka kukata tamaa ukiamini wewe huna bahati maishani mwako.
Nakuhakikishia kuwa hutapata matokeo ya utofauti mpaka pale utakapoanza kufanya kwa utofauti.
Mwanasayansi Albert Einstein alisema, “Insanity is doing the same thing, over and over again, but expecting different results” ikiwa na tafsiri kuwa ” ukichaa ni kufanya kitu kilekile kwa namna ileile lakini ukitarajia majibu ya utofauti”
Comfort zone ndiyo imekuwa changamoto kwako. Unafanya vitu vinavyokupa raha ….hataki kufanya kwa utofauti kwa sababu nje ya comfort zone kuna maumivu;
[ ] Hujiendelezi binafsi kwa sababu hujisikii kujifunza kwa kusoma vitabu.
[ ] Ukipata fedha unatumia yote bila kuweka akiba kwani hutaki kuvumilia mbegu iote na kuzaa matunda mengi baada ya muda mrefu.
[ ] Hutaki kutafuta wateja wapya kwa sababu unaogopa watakataa kununua.
[ ] Unapanga kufanya mambo madogo madogo yasiyosumbua akili yako kuwaza jwa ukubwa zaidi.
[ ] Hutaki kujizuia na anasa, ndiyo maana unakopa mikopo hata yenye riba kubwa ili ule bata.
Rafiki hakuna maajabu yatakayotokea maishani mwako kwa kung’ang’ania comfort zone (mazoea).
Kama unataka matokeo ya tofauti, anza kufanya kwa utofauti sasa bila kujali maumivu unayojisikia;
[ ] Anza kukua wewe kwanza kwa kujisukuma kujifunza vitu vipya.
[ ] Jisukume kufanya chochote unachogusa kwa ubora zaidi.
[ ] Jisukume kujilipa wewe mwenyewe kwanza angalau 10% ya kila kipato chako kabla hujawalipa wengine.
[ ] Acha matumizi ya anasa ili uanze upate fedha ya kuwekeza na baadaye ikuzalishie fedha nyingi zaidi.
[ ] Weka malengo makubwa zaidi ya uliyoyazoea kisha jisukume kuyafikia.
[ ] Jenga urafiki na kazi, tena kazi kubwa; kazi ni mwaminifu sana , atakulipa.
Rafiki anza kufanyia kazi haya, hakika utaanza kupata matokeo ambayo hujawahi kuyapata.
Kujifunza zaidi kisha kuchukukua hatua kubwa zitakazokuwezesha kupata matokeo makubwa unayostahili, hakikisha unakipata kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI.
Habari njema ni kuwa utakipata kitabu hiki leo kwa bei ya ofa ya pasaka. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kuwahi ofa yako.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz