Fedha Unazozitafuta Zimejificha Hapa. Hata Sasa Unaweza Kuanza Kuzitengeneza.
Unatafuta fedha kwa nguvu kubwa lakini huzioni au unaziona kidogo tu.
Unajiuliza fedha zimejificha wapi?
Kuna wakati umehisi fedha zimeitoroka dunia.
Lakini hakuna fedha iliyoiacha dunia.
Kuna maeneo mengi ambako fedha yako imejificha.
Leo nitakushirikisha eneo moja ambalo lipo karibu sana nawe ili uanze kuitengeneza fedha hiyo.
Fedha imejificha kwenye mawazo.
Rafiki! Kila kitu huanza kama wazo. Kitu chochote ambacho macho yako ya nyama yanakiona sasa, mwanzoni kilikuwa wazo.
Kumbe fedha zinaanza kama wazo.
[ ] Kumbe kama unataka fedha, anza kuwaza vema kwanza.
[ ] Kama unataka fedha zaidi, waza zaidi.
[ ] Mawazo sahihi yatakupa kitu sahihi cha kufanya kisha kupata fedha.
Kwenye mti kuna mbao.
Ndani ya mti kuna samani.
Ndani ya jiwe kuna sanamu.
Fikiri vizuri! Vitu vilivyokuzunguka vimeficha fedha.
- Simu yako imejaa wateja wa biashara yako. Anza kumpigia mmoja baada ya mwingine.
- Jokofu(friji) linalounguruma usiku kucha likiwa wazi kabisa linaweza kuweke vinywaji vya kuuzia majirani.
- ‘Oven’ unayotumia mara moja kwa wiki au mwezi kupikia mikate ya familia tu inaweza kutumika kupika mikate ya kuuza.
- Kuna vitu vizuri ulivyonavyo huvitumii au unavitumia mara chache, unaweza kuuza ukapata mataji wa kuanzisha biashara.
- Pikipiki unayoitembelea kwa muda mfupi sana inaweza kuwa bodaboda na ikakupatia fedha.
Chukua hatua;
Yatazame mazingira yaliyokuzunguka na vitu ulivyonavyo……vimeshikilia fedha kama utaamua kufikiri utaziona.
Wazo gani umelipata la kuanza kukupa fedha? Nishirikishe ili tuliboreshe zaidi.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz