Mafanikio Yako Hayapo Kwenye Matamanio Yako 1000 Bali Yapo Kwenye Kitu Hiki Kimoja…….


Categories :

Je umekuwa ukitafuta mchawi wa mfanikio yako lakini humpati! Je tayari umeshamsingizia jirani yako?

Unaweza ukafikiri hufanikiwi kwa sababu hujui nini ufanye, kama hilo ni kweli basi ambacho hujui kitakuwa hiki ninachokwenda kukueleza hapa.

Umesikia, umeona na kuhisi kisha kupata matamanio ya nini ukifanye maishani mwako.

Umetengeneza mipango mizuri na ukaona picha kabisa ya nini utaenda kukipata mwishoni.

Mbona muda uliotegemea upate mafanikio umeshafika lakini hatuoni matokeo yoyote hata dalili tu…..?

Hapo ndipo utagundua kuwa matamanio yako mazuri hata kama yatakuwa 1000 yanashindwa na kitu chenye nguvu….KITENDO KIMOJA.

Matamanio mengi, makubwa na mzuri hata yaliyoambatana na mipango mizuri ni bure kama hakuna VITENDO ndani yake.

Kama umekuwa ukitafuta mchawi wa mafanikio yako basi jua kuwa ni KUKOSEKANA KWA VITENDO KWENYE MIPANGO YAKO.

Kufanya kile ulichokitamani na kukipangilia bila kuruhusu sababu yoyote ile huitwa NIDHAMU KALI.

Nidhamu kali ndiyo koki itakayofungua matokeo kwenye maisha yako.

Chukua hatua hizi:

  1. Tambua na weka wazi kabisa nini unataka maishani mwako. Kipato sh?…kisha weka namna ya kukipata.
  2. Tafuta sababu itakayokusuma kuchukua hatua ulizopanga hata pale mambo yatakapokuwa magumu. Je ni hali duni ya kiuchumi kwenye familia yako? Je ni kutaka kuacha urithi au alama hapa duniani?
  3. Gawa hatua kubwa kwenye vipande vidogo vidogo.  Ambazo zitakuwa rahisi kuchukua.
  4. Chukua hatua hata ndogo huku ukiendelea kuilinda picha kubwa uliyoitengeneza.

Je yapi yalikuwa malengo yako ya mwaka 2024? Hatua gani umeshachukua? 

Acha kuendelea kuongeza matamanio tu, weka kazi sasa kwa kuanza kuchukua hata hatua moja ndogo  lakini endelea kwa msimamo.

anza LEO anza SASA anza NAULICHONACHO.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *