Haya Ndiyo Matundu Madogo madogo Uliyoyatengeneza na Yanazamisha Meli Ya Maisha Yako .
Je umekuwa ukihisi kuwa unajitahidi sana kupambania maisha yako lakini mwisho wa siku unaona mambo hayaendi?
Je umekuwa ukitafuta na kupata fedha lakini ukiulizwa ziko wapi, huwezi kuonyesha?
Je umeanzisha biashara lakini unaona kabisa haikui na kuna kila dalili kuwa inaenda kufa?
Je ukitafakari unajiona una muda mwingi wa kufanya mambo, lakini jioni ikifika huoni cha maana ulichofanya?
Rafiki! Kama haya yanatokeo kwako basi tambua kuwa hata meli yenye tundu dogo tu, lisipozibwa litaingiza maji kwenye meli hiyo na kuizamisha.
Kuna tabia ndogondogo lakini muhimu ambazo umekuwa ukizipuzia kila wakati. Hizo zimekuwa ni matundu madogo kwenye meli ya maisha yako.
Matunda hayo yamekuwa yakiingiza kushindwa kwenye maisha yako. Kama vile meli kubwa na nzito inavyoweza kuzamishwa na tundu dogo ndivyo unavyoweza kuzamisha maisha yako na tabia ndogondogo za kushindwa.
Ziba matunda haya yanayozamisha maisha yako ya mafanikio;
[ ] Kutokuwa na maono/malengo/mipango.
[ ] Kuchelewa kuamuka
[ ] Kutojali afya yako
[ ] Kutumia fedha bila bajeti
[ ] Kutumia kipato chote
[ ] Kutumia zaidi ya kipato chako
[ ] Biashara yako kukosa mfumo
[ ] Kutosoma vitabu
[ ] Kutofanya tathmini ya malengo yako
[ ] Kutoweka akiba
[ ] Kung’ang’ania kipato kimoja
[ ] Kuhangaika na mambo ya wengine
Je ni matundu gani tayari umeshayatengeneza ambayo ndiyo yanazamisha meli ya maisha yako taratibu?
Nishirikishe tuone namna ya kuyaziba kisha uendelee na safari ya kuamsha uwezo wako ili kufanya mambo makubwa kisha kupata matokeo makubwa unayostahili.
“You Deserve More”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz