Una Uhuru Wa Kuchagua,  Umechagua Nini?


Categories :

Kila kitu kinaanza kama wazo. Hivyo ulivyonavyo vimetokana na mawazo uliyotengeneza kisha matendo.

Kumbe ukitaka kubadili maisha yako , anza kwa kubadili namna unavyowaza.

Habari njema ni kuwa una uhuru wa nini ukiwaze na kubadili ulichokuwa unawaza.

[  ] Umewaza kushindwa una uhuru wa kuanza kuwaza unaweza.

[  ] Umekuwa ukiwaza kuwa wewe ni masikini sasa anza kuwaza kuwa wewe ni tajiri.

[  ] Umekuwa ukiwaza kuwa wewe ni dhaifu sasa anza kuwaza kuwa wewe ni imara.

[  ] Umekuwa ukiwaza kuwa wewe huwezi kuweka akiba…sasa anza kuwaza kuwa unaweza kuweka akiba hata kidogo.

[  ] Umekuwa ukiwaza kuwa wewe ni mtu wa kawaida, sasa anza kuwaza na kujiona wa thamani kubwa sana.

Usiwaze mara moja bali kila siku mpaka taswira hiyo injengeke ndani yako.

Usiishie kuwaza tu…sasa anza kufanya unayoyawaza….

Chagua mawazo hasi mawili ambayo yamekukwamisha kisha anza kuyawaza upande chanya….mara nyingine yatamke na kuyaandika…kisha anza kuchukua hatua hata ndogo juu ya mawazo hayo….

Wewe ni vile unavyowaza jiwazie mema na makubwa.

Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *