Jifunze Kwa Tai Ufanikiwe Sana.


Categories :

TABIA 6/7;

Hutengeneza kiota chenye miiba ili kuwafunza watoto wao.

[  ] Tai hutengeneza kiota chao sehemu ya juu sana ya miti ambako maadui hawafiki kirahisi.

[  ] Kiota chao huanza na matawi makubwa chini, miiba, vimti vidogo, majani laini, manyoya kisha miiba pembeni.

[  ] Ndipo jike hutaga mayai kuatamia na kutotoa vifaranga.

[  ] Kadri vifaranga vinapoendelea kukua tai huvisogeza pembeni kwenye miba ili iwachome na mara nyingine kutoka damu. Hufanya hivyo mara kwa mara.

[  ] Wakifikia hatua ya kuweza kuruka, wazazi hutoa kabisa manyoya na majani laini kwenye kiota ili wakutane na miiba ambayo maumivu yake huwalazimisha kutoka kwenye kiota na kuanza kuruka.


[  ] Maisha ya mafanikio yana changamoto zenye maumivu, jifunze uvumilivu ili upite vipindi hivyo kwa mafanikio.

[  ] Wafundishe wanao kukua hata kwa maumivu. Dunia ina mapito yote; raha na taabu. Naye atakuwa imara atakapobaki pekeyake.

“Utafanikiwa kutoka kwenye mazoea kisha kupiga hatua kubwa zaidi kama utakubali kuvumilia maumivu unayostahili”

Usikose Tabia ya 7/7 kesho.

Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *