Jifunze Kwa Tai Ufanikiwe Sana


Categories :

TABIA 7/7;

.

Tai akifikisha miaka 40 hufanya maamuzi magumu sana ili kuendelea kuishi .

[  ] Tai ana uwezo wa kuishi hata miaka 70

[  ] Lakini kwenye miaka 40 kucha zake huwa butu kuwinda, manyoya yake huwa mengi kushindwa kuruka;na mdomo wake huwa umepinda sana na butu kuwinda.

[  ] Ili kuendelea kuishi hutakiwa kufanya maamuzi magumu yenye maumivu.

[  ] Huenda sehemu yenye kificho ambako adui zake hawawezi kumfikia kisha kujinyonyoa manyoya yote, kujing’oa kucha zote na mdomo wake ili viote vipya.

[  ] Hatua hii huwa yenye maumivu makali lakini huvumilia kwa lengo la kuendelea kuwa hai.

[  ] Baada ya muda manyoya mapya, kucha na mdomo mpya huota na kumsaidia kuendelea kuishi miaka 70 au zaidi.


[  ] Kuna maeneo ya maisha yako yanasuasua kwa sababu vitu havikui tena.

[  ] Kuna tabia zimekuzuia na huwezi kukua tena.

[  ] Usipojitoa kuziacha tabia za kushidwa kisha kujenga tabia za mafanikio utakufa; mahusiano,  uchumi, afya nk.

[  ] Fanya maamuzi sahihi sasa ya kung’oa tabia za kushindwa hata kama zitakuwa na maamivu makali ili kupata nafasi ya kujenga tabia za mafanikio.
Tabia za kung’oa: Uvivu, kutojiendeleza, kuahirisha mambo, woga, matumizi mabaya ya fedha, kutoweka akiba, kutowekeza, kutotenga muda kwa ajili ya watu wako wa karibu……

Tabia za kujenga: Bidii katika kazi, kusoma vitabu, kufanya uliyopanga, kuwa jasiri, kweka akiba, kuwekeza, kuwa na muda mzuri na watu wako wa karibu…

Tabia gani utaanza kuzing’oa leo? Zipi utaanza kuzijenga leo ili kukuza mafanikio yako?

Hongera kwa kujifunza tabia 7 za tai. Ukiziishi hakika utapiga hatua kubwa maishani mwako.

Karibu sana.

Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *