Afadhali Kwenda Polepole Kuliko Hiki Unachokifanya……
[ ] Licha ya kutambua ana mwendo wa polepole, kobe naye hupanga safari zake kisha kufika.
[ ] Licha ya nyumba kutumia zaidi ya tofari elfu 10, fundi ujenzi hupanga tofari moja baada ya nyingine kisha nyumba kukamilika.
[ ] Licha ya mbegu ya mbuyu kutambua kuwa itahitaji miaka mingi ili kuwa mti mkubwa unaotishia macho ya watu, lakini hukubali kuanza kwa kuota na kukua taratibu.
Afadhali kwenda polepole kuliko kutokwenda kabisa ukihofia umbali wa safari.
Rafiki, safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja….
[ ] Anza biashara yako hata kwa udogo, hiyo ndiyo njia ya kufikia biashara ya ndoto yako.
[ ] Anza kuwekeza hata 1% ya kipato chako, hiyo ndiyo njia ya kuelekea kwenye uhuru wa kifedha
[ ] Anza kusoma vitabu hata kama kurasa moja, hiyo ndiyo njia ya kuwa na mtazamo na hatua bora.
[ ] Anza hata kwa kuongeza mteja mmoja tu kila siku kwenye biashara yako, hiyo ndiyo njia ya kukuza mauzo yako.
[ ] Anza hata kwa kujisukuma kufanya kitu kimoja kati ya vingi ulivyoviahirisha siku nyingi, hicho kitakuwa ufunguo wa kuwa mtu wa matokeo na siyo sababu.
Kitu gani unafikiri ukianza leo polepole na ukaendelea bila kuacha kitakufikisha kwenye ndoto zako?
Anza hicho LEO Anza SASA Anza na chochote ULICHONACHO.
Habari njema ni kuwa kitabu chako cha JENGA NIDHAMU KALI kitakusaidia kuianza safari ya mafanikio yako makubwa kwa kuthubutu kuchukua hatua ndogo kisha kuendelea.
Jipatie kitabu chako sasa.
Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 ili kujipatia nakala chache za ofa ya mwisho wa mwezi.
Karibu sana.
Mwl. Alfred Mwanyika
0752 206 899
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz