F2: Je Wewe Ni MJINGA, wa WASTANI au MWEREVU?….
Pata fedha tujue tabia yako…..naamini utakuwa umeshasikia msemo huu mara kadhaa.
Linapokuja suala la fedha watu hujitenga katika makundi matatu;
1. Wapotezaji(WAJINGA)
2. Watumiaji( WA KAWAIDA)
3. Wawekezaji(WEREVU)
Mtu akipata fedha huingia kwenye kundi moja wapo kati ya hayo….kwa hiyo ule msemo wa pata fedha tujue tabia yako tunaweza kuuboresha na kusema;
“Pata fedha tujue wewe ni Mjinga, Wa Kawaida au Mwerevu”
1. Wapotezaji(WAJINGA).
Hawa ni watu amabo wakipata fedha hutumia kununua vitu vya kutumia na kutupa tu au hata ambavyo hawavihitaji.
Fedha zao huishia kununua chakula, nguo ambazo nyingine hawa hawazivai, urembo na kucheza bahati nasibu…..
2. Watumiaji( WA KAWAIDA)
Hawa ni watu wenye vipato vikubwa wanavyovipata kwa kufanya kazi.
Hutumia fedha zao kununua vitu vinavyochukua fedha mifukoni mwao (liabilities) kama gari la kutembelea, nyumba ya kuishi,…..lakini pia huwa na bili kubwa kama umeme, maji, matengenezo.
Hawa hawafanyi uwekezaji wowote. Wakipata fedha wanatumia yote…wanafanya kazi tena wanapata fedha na kutumia yote…..miaka yote wapo palepale kiuchumi.
Wapo kwenye mashindano ya mbio za panya (Rat Race).
3. Wawekezaji(WEREVU)
Hawa ni wale ambao wakipata fedha hutenga kiasi fulani kwa ajili ya akiba na uwekezaji ndipo hutumia zinazobaki.
Kwa kufanya hivyo muda mrefu, uwekezaji wao hukua sana. Kuna muda hufika, fedha walizowekeza huzalisha fedha nyingine nyingi ambazo hutosha kumudu gharama zote za maisha ba ya wao kufanya kazi..
Hivyo kufikia uhuru wa kifedha .
Wewe rafiki yangu upo kundi lipi? Wapotezaji, watumiaji au wawekezaji?
Kundi ambalo unatakiwa kuingia kama bado upo hai ni la Werevu(wawekezaji). Kwa sababu kuna wakati hutaweza kufanya kazi kwa sababu ya maradhi, umri au sababu nyingine yoyote ile ni vizuri ukawa mwerevu wa kuwa na mpango wa kuwekeza ili fedha ziwe zinakufanyia kazi kwa niaba yako;
Kwa kuwa Mwerevu utawekeza fedha zako kwenye;
1. Ardhi/majengo
2. Hisa
3. Vipande
4. Hatifungani
Nk
Ili uweze kutoka kwenye kundi ulilopo sasa huna budi kubadili mtazamo wako juu ya fedha….
Kubadili mtazamo unahitaji maarifa sahihi ya fedha.
Maarifa haya yamekosekana kwenye elimu ya kawaida uliyoipata shuleni.
Habari njema ni kuwa kwenye kitabu chako cha SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA kimeeleza kiundani sana juu akili ya fedha unayohitaji kuijenga ili kuwa mwerevu juu ya fedha zako kisha kufikia uhuru wa kifedha.
Si hivyo tu, bali ukipata nakala hiyo utafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye programu ya STAAFU UKIWA HURU KIFEDHA ambapo utaongozwa hatua kwa hatua ili uwekeze kwa msimamo kisha kufikia uhuru wa kifedha.
Hii siyo fursa ya kuipoteza…
Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala ya kitabu chako cha SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA kisha kuingia kwenye programu ya STAAFU UKIWA HURU KIFEDHA .
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Trainer, Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz