Vichocheo Vitano(5) Vitakavyoifanya Biashara Yako Ikue


Categories :

“Hali ni  mbaya; 96% ya biashara zote hushindwa ndani ya miaka 10, huku 80% zikishindwa ndani ya miaka miwili ya kwanza “
Sabri Subi

Hii si habari  njema juu ya biashara yako. Naamini umeshuhudia biashara nyingi zikianzishwa kisha kufa ndani ya muda mfupi tu…..

Kile ambacho hakikui basi kinakufa. Hakikisha biashara yako inakua kila wakati. Ili biashara yako ikue inahitaji kuwa na vichocheo(hormones)..

Jifunze leo vichocheo vitano vya kuifanya biashara yako ibaki hai kisha kuendelea kukua.

1. Ukuaji binafsi
Biashara yako haiwezi kukua zaidi ya wewe ulivyo. Kama unataka biashara yako isife basi hakikisha wewe mwenyewe kwanza hufi….ikuze akili na imani yako kwanza juu ya biashara yako….jifunze kila siku.

2. Malengo
Weka malengo kwenye biashara yako ili yakuongoze. Unataka uuze sh kwa siku, wiki, mwezi? Unataka upate faida sh….? Unahitaji kufikia wateja wangapi kwa siku?

3. Nidhamu
Kwenye kila unachopanga kufanya, usiahirishe…acha visingizio.  Hakuna kazi hakuna mauzo!…hakuna fedha(damu). Fedha zikikauka kwenye biashara yako….biashara itakufa. Jisukume kutimiza malengo ya biashara uliyojiwekea.

4. Thamani
Watu watakupa fedha si kwa sababu wewe unazihitaji sana, hapana…kwa sababu wameioana thamani kwenye bidhaa au huduma unayoitoa.

Hakikisha bidhaa au huduma zako zina thamani kubwa sana pia unawashawishi wateja wako kuiona thamani hiyo..

5. Uvumilivu
Si kila utakachotakiwa kukifanya utakipenda…vumilia kukifanya kwa sababu kitakupa matokeo unayoyataka.
Kuna wakati matokeo yatachelewa, vumilia, kama unachokifanya ni sahihi…muda utakujibu…

Naamini unatamani biashara yako iendelee kuishi na kukua.  Anza sasa kujenga vichocheo hivi kwenye biashara yako.

Hata hivyo kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA ni mwongozo kamili wa kukusaidia kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa unayotarajia. Kimejaa mbinu za kuhakikisha unatoa thamani bora kwa wateja wako…utakuza mauzo yako ,kupata faida kubwa. Pia kitakusaidi njia kutunza na kukuza fedha zako.

Kama unataka biashara yako isiingie kwenye 96% za biashara nyingi zitakazokufa hivi karibuni …basi hakikisha umekipata kitabu hiki leo. Habari njema ni kuwa kitabu hiki utakipata kwa bei ya ofa. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.

Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Trainer,  Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *