Usiuangalie Udogo Wako Bali Upekee Wako…
Rafiki!
“Kilichomsaidia nyuki kugundua uwezo wake wa kipekee wa kutengeneza asali ni kutojilinganisha ukubwa wa umbo lake na tembo bali kujiuliza upekee aliokuwa nao kwenye umbo lake dogo”
Moja ya kosa kubwa ambalo umelifanya na limekuacha nyuma ni kujilinganisha na watu wengine.
[ ] Umeangalia makubwa wanayofanya wengine kisha umekata tamaa kwa kuona wewe si kitu.
[ ] Umeangalia hatua walizopiga watu wengine umeona wapo mbali sana…imekukatisha tamaa ya kuanza safari yako.
[ ] Umelinganisha ukubwa wa vipato vya watu wengine kisha ukahitimisha kuwa wewe utakufa masikini.
[ ] Umeangalia vipaji vya watu wengine na makubwa wanayoweza kuyafanya…umejiona wewe hukubahatika kuwa na kipaji
Ndugu! Ulinganisho huu ndiyo uliokugharimu na kukuacha hapo chini ulipo ambapo hustahili kuwepo hapo.
Nyuki aliushinda mtego huo wa kutotaka kujilinganisha ….hata alipomuona tembo hakutaka kuingia unyonge wa kujiona mdogo.
Nyuki aliachana na unyonge wa udogo wa umbo lake kwa kuutafuta upekee aliokuwa nao ndani ya umbo lake dogo.
Ndipo nyuki alipouona uwezo wa kipekee wa kutengeneza asali ambayo kila aliyopo duniani anashuhudia utamu wake.
Acha kujidharau..
Acha kujilinganisha
Acha kukata tamaa
Acha ndoto ndogo
Acha kuangalia nje
Ndani yako una nguvu za kipekee za kutengeneza asali ambayo dunia inaisubiri.
Kitu gani ambacho ukijaribu kukifanya kinakupa matokeo makubwa yanayoshangaza wengine angali wewe ukijiona umefanya kwa ukawaida tu?
Fokasi kwenye kitu hicho, huko ndiko upekee wako ulikojificha.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kimekuwa msaada kwa watu wengi kubadili maisha ya unyonge waliyokuwa nayo kisha kupata ujasiri wa kuamsha nguvu kubwa ambazo zililala tu ndani yao.
Ni zamu yako sasa. Jipatie nakala yako sasa ili utambue asali unayoweza kuitengenezea dunia na ikawa tayari kukulipa. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 ili kukipata kitabu hiki leo kwa bei ya ofa ya mwanzo wa mwezi.
Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Trainer, Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.