Maajabu Haya Unaweza Kuyatengeneza Maishani Mwako Pia.

’Vipande vya kioo vinaweza kukusanya miozi ya jua na kuiongezea nguvu kiasi cha kuweza kuunguza karatasi’’
Vipande vya kioo vikipangwa vizuri , huwa vinakusanya miale ya jua iliyotawanyika na kuiweka pamoja.
Kwa sababu kuna nishati kwenye kila mwale, inavyokusanywa, nishati hiyo huungana na kuwa na nguvu kubwa zaidi za nguvu ya mwale mmoja.
Nguvu hiyo ina uwezo wa kuunguza karatasi. Unaweza kufanya jaribio hilo hata nyumbani.
Haya ndiyo maajabu yanayotokea kwenye kuishi upekee.
Ukiona mtu amefanya makubwa ya kukushangaza basi jua alitoka nje ya kundi. Hakutawanyika huko na huko akifanya kila alichoona wengine wakifanya,
Bali alitoka nje ya kundi kisha kupata nafasi ya kuwa yeye na kusikiliza maoni ya sauti yake tu, na baada ya hapo alielekeza kila alichokuwa nacho kwenye jambo moja lililobeba maisha yake.
Kama unaiona idadi kubwa ya watu wakifanya mambo ya kawaida, tambua kuwa bado wapo kwenye kundi, wakisiliza maoni ya watu wengine.
Wanafanya kila au chochote wanachokutana nacho. Hii inatawanya nguvu zao na hivyo kupata matokeo ya kawaida.
Kila mtu ana nguvu ya asili ndani yake. Hii ni nguvu ya kipekee ambayo mtu anakuwa nayo tangu kuzaliwa kwake. Hii nguvu hujidhihirisha pale mtu anapoishi upekee wake, yaani kusudi lake.
Utanufaika na nguvu hii kama utasikiliza ndani yako nini ungetamani ukikamikishe ukiwa hapa dunia na nini unaweza kukifanya kwa ustadi mkubwa.
Huko sasa elekeza kila kitu; muda, nguvu, umakini na rasilimali zote….hapo ndipo maajabu yatatokea maishani mwako.
Uhakika nilionao ni kuwa wewe una vitu vya pekee unavyoweza kuvifanya. Na una sababu (kusudi) maalumu ….huko ndiko kwa kuelekeza miale ya kuleta maajabu.
Hata hivyo kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kitakusaidia wewe kutambua nguvu zako za kipekee kisha kuziamsha kufanya makubwa.
Umeuishi ukawaida kwa muda mrefu, tafuta na anza kuishi upekee wako sasa; bonyeza hapa kupata kitabu hiki; https://vitabu.somavitabu.co.tz/#/view/shop-item/66/
"2025 Unastahili Zaidi Ya Ulichokipata 2024"
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Scientist, Author &Trainer
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899