Hii Ndiyo Zawadi Yako Uliyokaa Nayo Muda Mrefu Bila Kuifungua.
Samaki alipozaliwa na kufungua sanduku lake la zawadi akaiona zawadi yake ya pekee na kuanza kuitumia mara moja. Zawadi hiyo ilikuwa uwezo wake wa kipekee wa kuogelea majini na kuyafurahia maisha hayo.
Kinda la ndege lilipototolewa lilianza kufungua sanduku la zawadi kisha likaona zawadi yake ya kipekee ya kuelea hewani na kufurahi anga. Alipokamilisha kufungua akaanza kuruka hewani kwa ufanisi mkubwa. Nyuki walipogundua zawadi ya pekee waliyopewa, waliifungua na kuanza kutengeneza asali tamu, bila kujali nani anaitumia.
Na wewe ndugu yangu una zawadi ya pekee ambayo ulifungashiwa tangu kuzaliwa kwako. Ulitarajiwa uifungue na uanze kuitumia kwa uaminifu kupata mafanikio makubwa kama aliyopata samaki majini, au ndege angani au nyuki kwenye mzinga. Zawadi yako ambayo umeibeba tangu kuzaliwa kwako ni uwezo wako wa kipekee ambao uliwekwa ndani yako. Hii ni zawadi ambayo ukifanikiwa kuifungua na kuitumia utafanikiwa kuyaishi maisha yako ya hapa duniani kwa ukamilifu.
Kila binadamu anazaliwa na uwezo wa pekee kwa ajili ya kuwezesha kufanya mambo mkubwa na kupata mafanikio makubwa. Lakini ni bahati mbaya kuwa binadamu wengi wanakufa na uwezo huo. Licha ya mambo makubwa yaliyofanyika na kukushangaza, lakini tafiti zinaonyesha binadamu ametumia wastani wa 10% ya uwezo wake. Kumbe makaburi yana hazina kubwa ya uwezo ambao watu wamekufa nao bila kuutumia.
Uwezo ni nguvu ambayo mtu anayo lakini haijatumika. Hata ndani yako una nguvu hiyo. Hiyo ndiyo zawadi uliyopewa, kinachosubiriwa ni wewe kuifungua, kuitambua na kuanza kuitumia. Hujaweza kuitumia zawadi hiyo, labda kwa sababu hufahamu kuwa unayo licha ya kuendelea kutamani na kuiga za watu wengine.
Uwezo wako wa pekee ni nguvu ambayo ungeweza kuitumia kuweka malengo makubwa na kuyatimiza. Pia ungeweza kuitumia kukuza kile kidogo ambacho kimekuwa hakikui licha ya kuwepo kwa muda mrefu. Huu ni uwezo ambao ungeweza kutoa thamani kubwa hapa duniani na kuacha alama hata baada ya kufa.
Jambo la kwanza unalopaswa kufanya ili uweze kunufaika na zawadi hii ni kuamini kuwa una zawadi hii ya uwezo ndani yako. Kuamini kuwa kuna nguvu ambayo huwa inakaa tu ndani ya mtu bila kutumika muulize yule aliyewahi kukimbizwa na simba, alipata wapi nguvu za kuruka kichaka kirefu vile na kushindwa kurudia hali ilipokuwa shwari?
Jambo la pili ni kutambua upekee wa uwezo wako. Licha ya zawadi ya uwezo wa kuogelea alionao samaki, lakini hawezi kuogelea mchangani. Ili uweze kufaidi nguvu hii lazima ujue wapi kwa kuitumia. Je ni kwenye uongozi? Je ni kwenye uandishi? Je ni kwenye unenaji au kufundisha? Tambua kisha anza kuitumia.
Jambo la tatu ni kuwa na vichocheo vya kuamsha uwezo huo. Moja ya kichocheo hicho ni malengo, tena malengo makubwa. Malengo yanatoa uelekeo wa wapi nguvu hizo zielekezwe.
Ndugu! Nafahamu kuwa umeishi na zawadi hii ya pekee yenye thamani kubwa kwa muda mrefu bila kuitumia kikamilifu. Umeishi maisha yenye mafanikio kiduchu kwa sababu ya kutotumia uwezo wako ambao tayari unao ndani yako. Umeweka malengo, lakini umeshindwa kutumia nyenzo hii ya uwezo kuyatimiza. Kilio chako kimesikika, nimekuandalia semina ya siku kumi ambayo itakusaidia wewe kufungua zawadi yako na kuanza kuitumia.
Mada ya semina hii ni JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwaka kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.
Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.
Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.
Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.
Asante kwa kujali,
Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz