Jifunze Siri Hii Kutoka Kwa Simba; Itakuwezesha Kupata Chochote Unachotaka.
Mnyamapori akimuona simba huona kifo machoni pake. Lakini habari ni tofauti kwa simba, yeye akimuona mnyamapori anaona ni kitoweo kilichokaribia mdomo wake. Hii ni sinema ya ajabu ambayo simba anaitengeneza. Ni siri gani simba anazo zinazomfanya wanyama wamuogope kiasi hicho?
Simba akiliona kundi la wanyama kama vile swala bila kujali idadi yao, huona ni kitoweo tu mbele yake. Huamini ni suala la muda tu kufika ili kuweza kupata chakula chake kizuri. Imani kubwa hii aliyonayo hutokana na tabia zake alizonazo ambazo anajua zitamwezesha kumpata mnyama yoyote. Unaweza kujifunza tabia hizi kwa simba kukuwezesha kupata chochote unachotaka.
Maono: Simba akimuona mnyama yoyote yule bila kujali ukubwa na ukatili wake, akili yake huona kitoweo. Haijalishi ugumu na vipingamizi ambavyo vinaweza kujitokeza, yeye huona kitoweo tu mbele yake. Huu ni mtazamo muhimu sana ili uweze kupata chochote unachotaka. Unaona nini mbele ya maisha yako. Matokeo gani unayaona miaka mitano, kumi au ishirini ijayo. Tengeneza maono yako na yaone yakitimia.
Ujasiri: Licha ya ukubwa wa mnyama kama tembo, bado simba huona kuwa hicho ni kitoweo tu. Huondoa hofu na kujiamini kuwa anaweza kupata kitoweo kizuri na kingi cha mnyama yoyote. Tembo ni mkubwa kwa umbo kuliko simba, lakini simba hatishwi na hilo. Huvaa ujasiri wa kupata kitoweo kutoka kwa mnyama yoyote yule. Hii ni siri kubwa ya kujifunza kutoka kwa simba. Usiogope kuziendea ndoto na maono yako kwa sababu ya ukubwa wake. Wewe ona matokeo tu kwenye mambo makubwa unayotarajia kuyafikia. Vaa ujasiri kupata makubwa.
Kuwatisha maadui na kuchagua mnyama mmoja. Hii ni tabia ya werevu anayoitumia kupata kitoweo kutoka kwa mnyama aliye kwenye kundi kubwa. Simba huwatishwa wanyama walio kwenye kundi kwa sauti yake na mwonekano wake ili watawanyike na kuweza kuchagua mnyama mmoja ambaye atamkimbiza mpaka ampate. Ndugu! Huwezi kufanya kila kitu, unahitaji uzisambaratishe fursa na kubakia na moja mpaka matokeo yake. Utapata chochote unachokitaka. Using’ang’anie kila fursa, zitakushinda.
Moja ya upendeleo uliopewa mwanadamu ni kuitawala dunia na viumbe vilivyopo. Lakini kwa nini simba anaonekana amefanikiwa zaidi kuliko wewe? Kwa nini anakuwa na ujasiri kuliko wewe? Ni kwa sababu ametambua ni nini alichonacho ndani yake na kukitumia. Amefanikiwa kutambua mbinu anazoweza kuzitumia kupata chochote anachokitaka. Na wewe una uwezo wa kupata chochote unachokitaka kwa kujifunza mbinu hizi kuamsha uwezo na kuutumia.
Kwa kutambua hitaji hili muhimu kwako ili uweze kupata chochote kama simba anavyoweza kupata mnofu wowote ule, nimekuandalia semina ya siku kumi ambayo itakufunza mbinu muhimu za kuzifahamu na kuzijenga ili uweze kupata chochote unachokitaka.
Mada ya semina hii ni JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.
Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.
Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.
Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki:
https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.
Asante kwa kujali,
Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz