Fanya Kilicho Sahihi Siyo Kile Unachokipenda.


Categories :



Ni tamaa ya watu wengi kutaka kupata mafanikio makubwa katika kipindi cha uhai wao. Safari ya mafanikio makubwa ni ngumu yenye changamoto nyingi. Muda mwingi itakuhitaji uweke kazi tena kazi kubwa.

Hii imekuwa sababu mojawapo ya watu wengi kurudia njiani katika safari hii. Kuna watu wengi wenye ndoto,malengo na mipango iliyokamili ya namna ya kufika kule wanakotarajia kufika, lakini ni wachache sana ambao wanatekeleza mipango hiyo.


Ili mtu aweze kupata mafanikio anayoyatarajia, ni lazima afanye jambo lilolo sahihi. Hii ni kanuni ya asili kuwa kwenye kila matokeo unayoyaona kuna visababishi vya matokeo hayo. Huwezi kupata matokeo hayo bila visababishi hivyo.

Wakati wa kuanza kuweka kazi kwa ajili ya mafanikio yako makubwa, ni wakati ambao mtu huwa anatakiwa kufanya vitu kwa usahihi yaani inavyotakiwa kifanywa bila kijali anavipenda au laa. Hapa ndipo watu wanapohitajika kubadili baadhi ya mazoea na kufanya kinachotakiwa. Kwa mfano unataka kukusanya mtaji kwa kuweka akiba huna budi kujenga nidhamu ha kuweka akiba kwenye kila kipato badala ya kutumia kipato chote. Hapa ndipo unapotakiwa kujilazimisha kuweka akiba kwenye kila kipato hata pale ambapo ungetamani fedha hiyo ununulie kitu fulani.

Unafanikiwa kufanya jambo lolote kwa kujirudiarudia kwa kujenga tabia. Hivyo kufanya kilichosahihi na si lazima uwe unakipenda, inakulazimu ujenge tabia za kukwezesha kufanya kwa uaminifu. Zifuatazo ni baadhi ya tabia zitakazokuwezesha kufanya kitu kwa sababu ni sahihi hata pale kinapotakuwa hakikufurahishi;

Nidhamu:Hi ni tabia ya kufanya kitu sahihi kwa wakati sahihi na kwa viwango sahihi. Hii ni tabia muhimu sana kama kweli unataka kufikia mafanikio yako. Kama umeshapanga malengo ya kutimiza malengo ya mwaka 2022, tambua kuwa itakuwa ni ngumu sana kuyatimiza kama hutajenga tabia hii muhimu ya kufanya kilicho sahihi.

Uwajibikaji: Ni rahisi sana kuacha kile unachokifanya kama hakikufurahishi na hukipendi. Na ili uweze kukifanya katika mazingira kama hayo huna budi kuona kuwa hilo ni jukumu lako na hakuna mtu mwingine wa kumuachia. Ndiyo maana inashauriwa sana kuweke mipango yako mingi inayoendana na kusudi lako, ambapo utaona kuwa kazi hiyo ni yako na unawajibika kwa asilimia mia moja kuitimiza.

Uvumilivu: Ili ufanye kilicho sahihi na kupata matokeo hata pale unapokuwa hukipendi kitu hicho, una hitaji uvumilivu. Matokeo yanapochelewa, unaweza kushawishika uachane na kile unachokifanya. Lakini kwa sababu unachokifanya ni sahihi, unahitaji kuendelea kufanya na kusubiri. Huu unaitwa uvumilivu.

Ndugu ili mwaka huu uwe wa mafanikio makubwa kwako huna budi kufanya kilichosahihi bila kujali unakipenda au la. Ili kuhakikisha unafanikiwa katika hilo mtandao wa AmshaUwezo umekundalia semina ya siku 10 ambayo itakuwezesha kutengeneza tabia za kufanya kilichosahihi na kukuwezesha kutimiza malengo yako ya mwaka 2022 na miaka mingine.

Mada ya semina hii ni  JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO. Katika semina hii utatmbua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia sa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *