Kama Kweli Unayapenda Maisha Yako Hutaacha Kufanya Jambo Hili.
Maisha ya binadamu hapa duniani yamebebwa na muda wa uhai wake. Hii ina maana kuwa mtu anaweza kufanya kile anachotamani kukifanya hapa duniani kwenye kipindi cha uhai wake tu. Baada ya kufa hawezi kufanya jambo lolote licha ya dunia kuendelea kuwepo.
Benjamini Franklin alisema “Do you love life? Then do not squander time, for that’s the stuff that life is made of.” Akimaanisha kuwa kama unayapenda maisha basi acha kupoteza muda kwani hicho ndiyo kitu pekee kinachotengeneza maisha yako. Maisha yako ni muda , hakuna muda hakuna maisha. Kwa hiyo kama kweli unayapenda na kuyajali maisha yako hutaacha kujali muda. Kujali muda ni kutokuwa tayari kupoteza muda wako kwa kufanya vitu visivyokuwa na umuhimu kwenye maisha yako.
Kuna mambo kama mwanadamu unatamani kuyafanya katika maisha yako. Mambo hayo yanabebwa na kusudi la maisha yako, ndoto unayotamani kuitimiza na malengo unayofanyia kazi. Haya yote yamebebwa na muda wa uhai wako. Utaweza kutimiza kusudi la maisha yako na kuishi ndoto yako kikamilifu kama utaanza kwa kujali muda ulio nao.
Huwezi kufikia maisha ya mafanikio kama hutaweza kutawala muda ulionao. Kwa kutumia vizuri muda wako ndipo utaweza kufanya vilivyo muhimu na kupata matokeo ambayo yatakuwa na faida kubwa kwako na watu wengine.
Licha ya umuhimu mkubwa wa muda kwenye maisha ya mtu, uongozi binafsi wa muda umekuwa changamoto kwa watu wengi. Binadamu wote tuna muda sawa, kila mtu ana masaa ishirini na nne kwa siku na siku saba kwenye kila wiki. Lakini licha ya usawa huo wa muda kwa watu wote, kuna tofauti kubwa sana kwenye mafanikio baina ya watu. Watu wawili wenye umri sawa wanaweza kuwa na utofauti kubwa wa mafanikio ya maisha yao. Sababu mojawapo kubwa ya tofauti hiyo ni matumizi ya muda.
Ndugu! Hali ya maisha uliyonayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na namna ya ulivyotumia muda uliokwisha kupita. Kama kuna mambo ulitamani uwe umeshayafanya na kupata matokeo yake lakini bado hujapata, sababu mojawapo ya kutoyapata ni jinsi ulivyotumia muda wako. Nini kinasababisha kutotumia muda wetu vizuri na kupata matokeo makubwa?
Mipaka ya akili zetu. Chochote ambacho akili inakipokea na kukiamini kinakuwa chako. Kumekuwa na dhana kuwa hakuna muda wa kutosha wa kufanya mambo ya maana na hivyo kufikiri kuwa huwezi kufanya kitu cha maana hapa duniani. Mwanafalsafa Seneca alisema kuwa “It is not that we have a short space of time, but that we waste much of it. Akimaanisha kuwa si kuwa tuna muda mfupi wa maisha bali tunapoteza muda mwingi. Tuna muda wa kutosha wa kufanya mambo yenye umuhimu kwenye maisha yetu, lakini watu wengi wanaupoteza kwa mambo yasiyo na umuhimu kwenye maisha yao. Acha kufikiri ufinyu wa muda, una muda wa kutosha wa kufanya mambo yenye umuhimu tu.
Kukosa vipaombele. Hakuna muda duniani wa kufanya kila kitu. Una muda pekee wa kufanya yale ya muhimu. Huwezi kuacha kufanya kila kitu kama huna vipaombele. Vipaombele vitatokana na vile ulivyo na hamu kubwa kuvikamilisha kipindi cha uhai wako. Utaweza kuweka vipaumbele kwa kutambua kwanza kusudi la maisha yako, ndoto yako na malengo ya kufanyia kazi.
Una muda mwingine wa mwaka 2022. Una nafasi ya kutumia muda wako vyema na kupata matokeo makubwa kwa kuwa na vipaumbele na nidhamu ya kuishi vipaumbele hivyo. Kuhakikisha unajenga tabia hii muhimu mtandao wa AmshaUwezo umeandaa semina ya siku kumi ambapo somo mojawapo litakalofundishwa ni matumizi sahihi ya muda ili kupata mafanikio makubwa. Kupata fursa hii muhimu, jiunge leo na kundi hilo maalumu la semina kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
Mada ya semina hii ni JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU MALENGO YAKO. Katika semina hii utatambua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.
Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.
Gharama za semina hii ni shilingi elfu tano tu (5,000/) kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.
Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/lvfrgvlqf3kdeh5klocvqc
kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.
Asante kwa kujali,
imeandaliwa na alfred mwanyika
kocha na mwalimu wa uwezo wako halisi
mawasiliano;
simu; 0752206899/0714301952
barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
tovuti: www.amshauwezo.co.tz