Jinsi Unavyoweza Kutumia Kanuni Ya Tatu Ya Mwendo Ya Newton Kuboresha Miasha Yako .
Isaac Newton ni miongoni mwa wanasayansi nguli waliowahi kutokea hapa dunia. Mwanasayansi huyu atakumbukwa sana kwa mchango mkubwa wa tafiti zake kwenye mwendo na nguvu. Moja ya sheria za mwendo alizozigundua ni sheria ya tatu ya mwendo ya Newton inayosema “To every action there is ana equal anda opposite reaction” akimaanisha kuwa kwenye kila kitendo kinachofanyika kuna nguvu nyingine sawa inayozalishwa lakini katika uelekeo kinyume.
Hii ni sheria muhimu sana tunayoweza kuitumia katika maisha yetu kupata matokeo tunayoyataka. Newton anasema kwenye kila nguvu unayoweka kuna matokeo yanayotokea yaliyo sawa kwenye uelekeo tofauti.
Maisha ya mtu ya mafanikio ni maisha ya matokeo, huwezi kupiga hatua bila kuwa na matokeo. Newton anatukumbusha kuwa ili uweze kupata matokeo lazima uweke kitendo kwanza. Pia ili uweze kupata matokeo makubwa, vitendo havina budi kuwa vikubwa.
Vitendo vilivyopo kwenye sheria hii ya tatu ya mwendo ya Newton ni thamani ambayo mtu anaitoa kwa watu wengine. Matokeo sambamba aliyoyasema Newton ni mrejesho ambao watu wanaweza kukupa baada ya wewe kuwapa thamani.
Hii inaendana na kauli aliyoisema Zig Ziglar kuwa “You will get all you want in life, if you help enough other people get what they want.” akimaanisha kuwa utapata chochote kwenye maisha kama utawasaidia wengine vya kutosha kupata wanachokitaka. Kupata mafaniko makubwa katika maisha yako kunaenda sambamba na kutoa thamani kubwa kwa watu.
Lengo la awali la biashara yako inabidi liwe kuwapa thamani watu wengine. Kadhalika lengo la awali la huduma unayotoa inabidi iwe kuwapa thamani kubwa watu wengine. Hili limekuwa tatizo kwa watu wengi. Wengi wameshindwa mafanikio makubwa kwa sababu wamejitanguliza wao kwanza kwenye vile wanavyovifanya. Unamkuta mfanyabiashara anatangulia kuitaka fedha ya mteja badala ya kufikiri kwanza kuhusu thamani anayoitoa kwa watu wengine.
Ndugu nafahamu wewe ni miongoni mwa watu wenye matamanio ya mafanikio makubwa. Ili kufikia hilo naamini umeshaweka malengo ya nini unaenda kukifanya mwaka huu. Newton anakukumbusha kuwa ili uweze kupata matokeo makubwa huna budi kuwa na vitendo vikubwa ambayo ni thamani unayowapa.
Kumbe ili uwe na mwaka wa mafanikio 2022 huna budi kujenga tabia ambazo zitakuwezesha kutoa thamani kubwa kwa watu wengine. Kwa kutambua uhitaji huo mtandao wa AmshaUwezo umekuandalia semina ya siku kumi iliyosheheni masomo yatakayokuwezesha kujenga tabia zitakazokuwezesha kutoa thamani kubwa kwa watu wengine na kukuwezesha wewe kupata mafanikio makubwa sana mwaka huu na miaka mingine. Jiandikishe leo ili kutoikosa fursa hii muhimu.
Mada ya semina hii ni JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU MALENGO YAKO. Katika semina hii utatmbua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.
Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia sa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.
Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.
Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.
Asante kwa kujali,
Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz