Ukiifahamu Kanuni Hii Utapunguza Kuwa ‘Busy’ Lakini Utapata Matokeo Makubwa Zaidi.


Categories :



Dunia ipo busy, kila mtu yupo busy. Kila mtu analalamika kuwa mambo ni mengi muda ni mchache. Wapo ambao wanatamani siku ingeongezewa muda, yaani iwe na masaa zaidi ya ishirini na nne.

Kuna wakati umefika umeamini kuwa unashindwa kupata matokeo makubwa kwa sababu ya ufinyu wa muda. Umeamini kuwa ungeongeza idadi ya kazi unazozifanya ungeweza kupata mafanikio makubwa zaidi, hivyo kuamini muda ulionao hautoshi.

Lakini kuna kanuni moja utajifunza leo ambayo itakuwa dawa ya ufinyu wa muda uliokutesa siku nyingi. Kanuni hiyo ni ya Pareto(80/20) inayosema “for many outcomes, roughly 80% of consequences come from 20% of causes”, ikimaanisha kuwa kwa matokeo mengi yanayotokea takribani 80% ya matokeo hayo yanatokana na 20% ya visababishi. Kwa lugha nyingine 80% ya matokeo unayoyapata maishani mwako yanatokana na 20% ya kazi/jitihada zote unazozifanya. Hivyo kun 80% ya kazi unazozifanya zinachangia 20% ya matokeo.


Kama una vyanzo 10 vya mapato basi ujue 80% ya mapato au faida unayoipata inatokana na 20% ya biashara zako, yaani biashara 2 tu. Hata kwenye shughuli za kila siku, ni asilimia 20% tu ya kazi zote utakazofanya zitakupa 80% ya matokeo utakayoyapata.

Kumbe ndugu kuna kazi nyingi sana tunazozifanya zenye mchango mdogo sana kwenye matokeo ya maisha yetu. Kumbe kuna 80% ya kazi tunazozifanya zinachangia 20% ya matokeo. Hizi 80% za kazi ndizo zinazotufanya tuwe busy. Mara nyingine tumepoteza muda mwingi kwenye kazi hizi ambazo hazina mchango mkubwa. Kanuni hii inakusaidiaje kupiga hatua kubwa zaidi ya hapo ulipo?

Kuainisha kazi zenye mchango mkubwa kwenye maisha yetu. Kaa chini kisha tafakari kazi zote unazozifanya kwenye siku. Baada ya hapo tathmini kwa kina ni kwa kiasi gani kila kazi unayoifanya imechangia kwenye mafanikio uliyoyapata.

Kuweka Vipaombele. Baada ya kutambua kazi zinazokupa matokeo makubwa kwenye maisha yako, huna budi sasa kuweka vipaombele. Kazi zile(20%) zinazochangia 80% ya matokeo inabidi zipewe muda, nguvu na umakini wako kwanza kabla hujafanya zile zenye mchango mdogo. Muda wa asubuhi ambapo unakuwa bado una nguvu na umakini mkubwa panga kufanya vile vipaombele kwanza.

Kwenye malengo yako ya mwaka huu ni 20% ya malengo hayo yatakupa 80% ya matokeo yote utakayoyapata. Kazi ya kwanza ambayo inabidi uifanye, ni kutambua hiyo 20% ya malengo yako. Ili iwe rahisi kwako kuiishi kanuni hii muhimu, mtandao wa AmshaUwezo umekuandalia semina ya siku kumi ambayo kanuni hii ya Pareto ni miongoni mwa masomo yatakayofundishwa kwa kina ili uweze kutumia muda wako kwenye vipaombele vitakavyokupa mafanikio makubwa.

Mada ya semina hii ni  JINSI YA KUAMSHA UWEZO WAKO ILI KUTIMIZA KIKAMILIFU  MALENGO YAKO. Katika semina hii utatmbua uwezo wako wa kipekee ulio nao ndani yako. Huu utakuwa mtaji wako wa kwanza wa kuanza kufanya makubwa. Pia utajifunza namna ya kutumia uwezo huo kutimiza malengo yako. Huu utakuwa mwanzo wa kumaliza mwako kwa furaha kubwa baada ya kufanikiwa kupata matokeo makubwa tofauti na miaka mingine.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao, (kundi maalumu la wasap). Itaanza tarehe 01 Machi, mpaka tarehe 10, Machi 2022. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku, utalisoma na kuchukua hatua zinazotarajiwa na kisha jioni kuanzia sa moja mpaka saa tatu usiku kutakuwa na majadiliano ya somo husika.

Gharama za semina hii ni sh 5,000 kwa siku zote kumi. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani ya masomo haya. Lakini kwa sababu nakujali sana wewe ndugu yangu, natamani usikosoke fursa hii muhimu ya kufanya mapinduzi kwenye maisha yako.

Ili usiweze kuipoteza nafasi hii, nakuomba leo hii ujiunge na kundi hili hata kabla ya kulipia ili ujipatie uhakika wa nafasi chache zilizopo. Kujiunga na kundi hili maalumu la wasap bonyeza kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/LvfrGvlqf3KDeh5kLocvQC
Kwa maelezo zaidi piga namba 0752206899/0714301952.

Asante kwa kujali,

Imeandaliwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *