Hii Ndiyo Siri Inayowatofautisha Waliofanikiwa Na Wasiofanikiwa, Itambue Na Kuitumia Leo.
Licha ya watu wengi kuwa na hamu ya kupata mafanikio makubwa, lakini wanaofanikiwa ni wachache sana. Watu wachache tu ndiyo walioshikilia mafanikio makubwa ambayo dunia imeyapata mpaka sasa. Watu wasiofanikiwa wamekuwa wakiwaona watu waliofanikiwa kama ni watu wenye bahati ambayo wao hawana. Wengine wamekuwa wakiwaona kama hawa watu wana kitu fulani ndani yao walichopendelewa ambacho wako hawana.
Ukweli ni kuwa hizo sio sababu za msingi zinazosababisha waliofanikiwa wapate hayo mafanikio. Lakini kuna siri moja kubwa inaowafanya waliofanikiwa kupata matokeo wanayoyapata, siri hiyo ni maarifa sahihi. Watu waliofanikiwa wanajua kuwa maarifa ndiyo mwanga wa kuwaongoza wapi waende na wanaendaje. Wanahakikisha kila siku wanajifunza ili kupata maarifa sahihi.
Mafanikio hayapatikani kwa kufanya kitu chochote bali kile kilicho sahihi. Wote waliofanikiwa wanafahamu kitu gani ni sahihi inawapasa wakifanye kisha wanakifanya. Watu walioshindwa wanafanya kitu chochote, na kisha kuishia kutopata mafanikio au matokeo ya kawaida.
Licha ya vitu vingi wanavyovifahamu, waliofanikiwa wanaamnini bado kuna nafasi ya kujifunza vitu vipya kila siku. Kwenye kila kitu wanachokifanya wanaamini kuna nafasi ya kufanya kwa ubora zaidi. Ubora huo utapatikana kwa kujifunza na kupata maarifa zaidi.
Kuyapata maarifa hayo, waliofanikiwa wanahakikisha wanasoma kila siku, wanahudhuria semina na mafunzo mbalimbali mara kwa mara. Licha ya elimu walioipata kwenye mfumo rasmi wa elimu, waliofanikiwa wanakuwa na hamu kubwa sana ya kujifunza zaidi. Hizi ni faida ambazo waliofanikiwa wanazipata kwa kutafuata maarifa kila siku ambazo na wewe unaweza kuzipata pia na kupiga hatua;
Wanajua kwa usahihi wanachokitaka. Kadri waliofanikiwa wanavyopata maarifa mbalimbali na sahihi ndipo wanapotambua nini hasa wanataka maishani mwao. Kwa kupitia maarifa, utatambua kuwa ili ufanikiwe lazima ujue kwa wazi kabisa ni kitu gani unakitaka maishani mwako. Hapo ndipo utachukua jukumu la kujua nini hasa unataka maishani mwako.
Unatambua njia sahihi za kupata unachotaka. Kuna watu wanafahamu nini wanakitaka maishani mwao, lakini kwa kutokuwa na maarifa ya kutosha wanashindwa kujua njia sahihi ya kukipata kitu hicho. Kwa kutafuata maarifa kama vile kusoma vitabu utakutana na watu wengine waliofanya/wanafanya kitu kama kile unachokifanya wewe. Kwa kusoma historia zao unaweza kujua njia walizotumia na wewe njia hizo kupata matokeo badala ya kuanza kujaribu ambazo huna uhakika kama zitatoa matokeo mazuri au la.
Umebaki hapo ulipo kwa muda mrefu sasa kwa sababu ya kuona unafahamu kila kitu. Umeendelea kufanya kwa mazoea baada ya kuendelea kufahamu vitu vile vile kila siku. Hata kitabu kitakatifu (kitakatifu) kinasema, ‘’Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa’’ (Hosea 4:6). Kama unataka kutoka hapo ulipo na kupiga hatua zaidi kwenye eneo lolote la maisha yako, huna budi kuanza kupata maarifa zaidi ya vile unavyovifahamu sasa. Sehemu nzuri ya kuanzia kupata maarifa kisha kuchukua vitendo na kupiga hatua ni kusoma vitabu. Kwa kusoma vitabu utapata maarifa ambayo yatakusaidia kubadili mtazamo wako na kuboresha maisha yako.
Kuna vitabu vingi sana vimeshaandikwa na watu mbalimbali kwenye kila eneo la maisha yako. Vipo ambavyo unaweza kuvipata bure kabisa kwa kupakua kwenye mtandao. Vipo vingine ambavyo unaweza kununua na kuvisoma. Panga leo kuanza kusoma kurasa tano mpaka kumi kila siku. Kwa kufanya hivyo utafanikiwa kusoma kitabu kimoja kila mwezi ambapo ukitumia maarifa utakayoyapata utapiga hatua kubwa sana.
Ili kuweza kupata maarifa sahihi yatakayokuwezesha kupiga hatua, mtandao wa AMSHA UWEZO unakukaribisha kwenye kundi maalumu na la kudumu la wasap litakalo kusaidia kupata maarifa kisha kupiga hatua na kufikia mafanikio yako makubwa. Kwa kujiunga na kundi hilo utapata
1. Mafunzo mbalimbali kama semina
2. Usimamizi wa malengo yako
3. Miongozo kama Kutambua kusudi lako, kuweka na kutimiza malengo
4. Makala na dondoo kila siku
5. Hamasa, kwa kuwa karibu na watu sahihi
6. Uchambuzi wa vitabu
Ada ya kujiunga na kundi hili ni shilingi elfu kumi (10,000/) tu, ambayo unaweza kulipa kwa awamu mbili. Ada hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani kubwa utakayoipata, lakini lengo lake ni kuhakikisha huikosi nafasi hii muhimu maishani mwako kwa sababu ya gharama. Hii siyo ya kuikosa, chukua hatua leo.
Bonyeza kiunganishi hiki kujiunga
https://chat.whatsapp.com/Dx1HF02stFq2LxIqoRTAUD
Kwa maelezo zaidi piga 0752 206 899/0714 301 952
(Mwl. Alfred Mwanyika)
“Wekeza kwenye Maarifa Timiza Malengo Yako”